TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSUDIO LA KUFUTA LESENI YA KAMPUNI YA MYCELL COMPANY LIMITED

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, ambayo inajulikana kwa kifupi kama TCRA ni taasisi ya usimamizi iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania namba 12 ya mwaka 2003. Mamlaka inayo majukumu mbalimbali ya usimamizi ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutoa na kufuta leseni za mawasiliano.

Tarehe 21 Novemba, 2008, TCRA ilitoa kwa kampuni ya Mycell Company Limited leseni kwa ajili ya kujenga miundombinu kitaifa (National Network Facilities Licence), leseni ya kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo (Network Services Licence), leseni ya kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano (Application Services Licence) na leseni ya kutumia masafa ya mawasiliano (Radio Frequency spectrum usage Licence).

Tarehe 27 Januari 2016 TCRA ilitoa amri ya utekelezaji kwa kampuni ya Mycell Company Limited kwa kukiuka masharti ya leseni walizopewa na pia kwa kushindwa kutoa huduma kinyume cha kifungu 21 (a) na (b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.

Kampuni ya Mycell Company Limited imeshindwa/imeacha kuchukua hatua kurekebisha ukiukwaji huo wa masharti ya leseni.

TCRA inaarifu umma kuhusu kusudio la Mamlaka la kufuta leseni za Mycell Company Limited za kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao na kutumia masafa ya mawasiliano.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Mawasiliano Towers
Na 20 Sam Nujoma
S.L.P. 474
14414 DAR ES SALAAM

Contact Details

20 Sam Nujoma Road
+255 22 2199760-8 More +

Staff Mail

isotext

Connect with us

Useful Links

  • used jeep for sale canada