TAARIFA KWA UMMA

UCHELEWAJI WA MALIPO YA MADENI SUGU YA ADA NA TOZO ZA LESENI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ni chombo cha Serikali kilichopewa jukumu la kusimamia Sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania. Majukumu ya Mamlaka ni pamoja na kutoa leseni na kusimamia makampuni ya mawasiliano, ikiwemo makampuni yanayotoa huduma za simu, utangazaji, huduma za intaneti, huduma za posta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto.

Katika kipindi cha muda mfupi, sekta ya Mawasiliano imekuwa kwa kasi sana nchini na kupelekea kuwepo watoa huduma wengi wenye leseni. Mamlaka imetoa leseni kwa wanaotoa huduma za mawasilianao nchini zikiwemo Leseni 22 za Miundombinu ya mawasiliano, Leseni 17 za kutoa huduma za mawasiliano, Leseni 85 za huduma za nyongeza za mawasiliano, Leseni 154 za huduma za utangazaji ambapo 128 ni za radio na 26 za Televisheni. Hali kadhalika Mamlaka imetoa leseni zingine 47 za kutoa huduma za Posta na Huduma za kusafirisha Vifurushi na Vipeto.

Kumekuwa na tatizo la baadhi ya watoa huduma kutolipa ada na tozo za leseni kwa wakati. Madeni mengine ya ada na tozo ni ya muda mrefu. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekuwa inafuatilia kwa karibu malipo ya ada na tozo za leseni kwa watoa huduma za mawasiliano waliopewa leseni kutoa huduma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Licha ya Juhud

Hatua kadhaa zimechukuliwa na Mamlaka ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa umma kuwakumbusha mara kwa mara watoa huduma wanaodaiwa kulipa ada na tozo wanazodaiwa. Kuanzia Januari 2016 Mamlaka ilikutana na watoa huduma wenye madeni sugu ama ya muda mrefu na kuwapa masharti ya jinsi ya kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo.

Jitihada hizo zimefanikisha kukusanya madeni ya ada na tozo za kiasi cha shilingi bilioni 19.1 hadi kufikia tarehe 31 Mwezi Machi 2016. Jitihada hizi zinaendelea kuhakikisha wadaiwa wote sugu wa Mamlaka wanalipa madeni yao yote.

Watoa huduma za Mawasiliano kutokulipa ada na tozo za leseni kunasababisha kutokuwepo na ushindani sawia kati ya watoa huduma katika sekta ya Mawasiliano na kusababisha kuonekana kuwepo na upendeleo kwa baadhi ya watoa huduma pamoja na kuikosesha Serikali mapato yake halali. Hali hii pia inasababisha kudumaa kwa Sekta ya Mawasiliano. Kutokulipa kwa muda ada na tozo za leseni ni uvunjwaji mkubwa wa masharti ya leseni kwa mujibu wa sehemu ya 21(g) ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic and Postal Communications Act - EPOCA) Kifungu cha 306 cha sheria hiyo, ambayo yanaweza kusabisha mtoa huduma kufutiwa leseni.

Mamlaka ya Mawasiliano inaendelea kuchukua hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kusimamisha watoa huduma kutokutoa huduma au kuzifuta leseni zao, kukusanya madeni wanayodaiwa kwa njia zingine za kisheria ikiwa ni pamoja na kuteuliwa kwa kampuni ya kudai madeni(debt collector) kwa watoa huduma watakaoshindwa kutimiza ahadi zao kama walivyokubaliana na Mamlaka. Watoa huduma 18 waliosimamishwa leseni zao au kunyanganywa leseni wameshawasilishwa kwa mdai madeni aliyeteuliwa na Mamlaka ili kukusanya madeni hayo sugu.

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kukusanya mapato yake, Mamlaka inapenda kuwakumbusha na kuwaonya watoa huduma ambao bado hawajalipa madeni yao kufanya hivyo haraka kama walivyoahidi kabla Mamlaka haijachukua hatua zaidi za kisheria za kufutiwa leseni na kukabidhiwa kwa kampuni ya kudai madeni. Aidha, tunasisitiza umuhimu wa watoa huduma za Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanatimiza Sheria, Kanuni na Mashati ya leseni zao kwa kulipa ada na tozo wanazodaiwa kwa wakati.

IMETOLEWA NA;

Dr. Ally Y. Simba
MKURUGENZI MKUU
7 Aprili, 2016

Contact Details

20 Sam Nujoma Road
+255 22 2199760-8 More +

Staff Mail

isotext

Connect with us

Useful Links

  • used jeep for sale canada