JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Majedwali ya Ugawaji wa Masafa wa Kitaifa (NFAT) yanaelezea jinsi bendi mbalimbali za masafa zinavyotumiwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yanatoa mfumo ambao utoaji wa masafa unapaswa kufanywa kwa huduma zote za redio nchini. NFAT inaweza kurekebishwa kufuatia mabadiliko katika maamuzi ya leseni ya Mamlaka, au kwa kuzingatia mabadiliko katika Sheria za Redio yaliyofanywa na Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Redio (WRC) wa Muungano wa Mawasiliano ya Kimataifa (ITU) na jinsi yanavyoathiri ugawaji, au kufuatia maamuzi mengine ya kitaifa kuhusu wigo wa masafa.

1. Jedwali La Mpangilio Wa Masafa Kitaifa, 2022

2. Jedwali La Mpangilio Wa Masafa Kitaifa, 2020

3. Jedwali La Mpangilio Wa Masafa Kitaifa, 2017

4. Mpango wa Ugawaji wa Masafa Afrika

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!