JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Maombi ya leseni ya Vifaa vya Miundombinu, Leseni ya huduma za miundombinu, Leseni ya matumizi ya huduma za miundombinu kutoa huduma za kielektroniki na Leseni ya huduma ya maudhui kitaifa yanapitia mchakato unaozingatia umakini wa uwasilishaji kama ifuatavyo:

  1. Mamlaka itatangaza kwa vipindi maalum tarehe za mwisho za kuwasilisha maombi.
  2. Maombi yatakayopokelewa yatapangwa kufuatia aina ya leseni inayoombwa; yaani leseni ya Vifaa vya Miundombinu, Leseni ya huduma za miundombinu, Leseni ya matumizi ya huduma za miundombinu kutoa huduma za kielektroniki na Leseni ya huduma ya maudhui na soko ambalo leseni husika inaombwa, yaani Kimataifa, Kitaifa, Mkoa, Wilaya na Jamii.
  3. Maombi yatakayopokelewa yatachambuliwa kuona iwapo yana viambatanisho vyote vinavyotakiwa, ambavyo ni: risiti ya ada ya maombi, fomu iliyojazwa kikamilifu, mpango wa biashara, mpango wa kueneza huduma, usajili wa kampuni, taarifa kuhusu mipango ya kiufundi ya huduma itakayotolewa, taarifa kuhusu uzoefu wa mwombaji na wasifu wa kampuni.
  4. Waombaji ambao maombi yao hayakidhi vigezo wataarifiwa kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa. Wanaokidhi vigezo wataarifiwa kwa utaratibu uliowekwa.
  5. Mamlaka inafanya uchambuzi wa kina wa maombi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kwa kila aina ya leseni.
  6. Orodha ya waombaji itachapishwa kwenye magazeti yanayosambazwa kwa wingi na kuwekwa kwenye tovuti ya Mamlaka na kukaribisha maoni kutoka kwa umma.
  7. Timu ya uchambuzi itakutana na kutathmini maoni ya umma kwa kila mwombaji, ikiwa ni pamoja na kuwahoji waombaji kuhusiana na maoni hayo iwapo kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.
  8. Mapendekezo ya timu ya uchambuzi yatawasilishwa kwa Menejimenti ya Mamlaka kwa ajili ya uamnuzi.
  9. Mapendekezo ya menejimenti yatawasilishwa kwenye Bodi kwa idhini.
  10. Mapendekezo ya Bodi yatawasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana ya sekta husika kwa mashauriano.
  11. Leseni zitatolewa kwa waombaji watakaofanikiwa baada ya kulipa ada stahiki (Ada ya awali, ada ya matumizi ya masafa, namna na kadhalika).

     Utaratibu wa kuwasilisha maombi ya leseni umefupishwa kwenye mchoro (uko kwenye mfumo wa PDF). Bonyeza hapa kupakua

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!