JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Mkutano wa Watoa Huduma za Mahudhui na Wadau Wengine Katika Kanda ya Kati ya TCRA, Dodoma 28 July 2021.


Mkutano wa Watoa Huduma za Mahudhui na Wadau Wengine Katika...

 

SEKTA YA UTANGAZAJI YA HIMIZA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI

Serikali imehimiza watoa huduma za Mawasiliano Nchini, kuzingatia Sheria na Kanuni zilizomo kwenye Leseni katika Utoaji wa huduma husika kwa Wananchi.

Akizindua kikao cha Watoa Huduma za Utangazaji na Maudhui Jijini Dodoma Tarehe 28-07-2021, wadau kutoka Azam Media, Multchoice Tanzania limited, Watoa Huduma kwa njia ya Cable, COSOTA na TFF na baadhi ya washiriki waliohudhuria ambapo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri K. Bakari, amesema baadhi Kanuni za Maidhui na Utangazaji zinafanyiwa maboresho na zinatarajia kuanza hivi karibuni

Dkt. Jabiri amesema kuwa TCRA imeboresha utendaji kazi zake kwa kuweka mifumo madhubuti zaidi na imeendelea kutoa ushauri kwa watoa huduma kila mara. Kikao hicho shirikishi pia kilihudhuliwa na watoa huduma za utangazaji na maudhui kutoka vyombo vya habari mbalimbali.

Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya kati, kililenga kutoa elimu ya namna bora zaidi katika kufikisha maudhui kwa walaji bila kuwa na migongano baina ya watoa huduma. Pia kikao kimependekeza wanaochakata maudhui kuangalia namna nzuri zaidi ya kuzuia maudhui yasiyo na staha kwa Jamii ili kuondoa malalamiko ndani ya Jamii.  

Kikao kimependekeza pia vikao kama hivi viwe vinafanywa mara kwa mara ili kuongeza ufahamu zaidi kwa watoa huduma na Mamlaka za Serikali zinazosimamia sekta ya maudhui ya Utangazaji.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!