TCRA

TCRA

Creating a Level Playing Field

Initializing...

HUDUMA ZA POSTA

Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 (TCRA Act 2003) ndio iliyoanzisha kanuni za Sekta ya Posta ambapo TCRA imepewa jukumu la kusimamia utoaji wa huduma za Posta ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria ya TCRA inazuia ufanyaji wa shughuli za Posta bila ya leseni halali inayotolewa na TCRA,…

HUDUMA ZA POSTA

Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003 (TCRA Act 2003) ndio iliyoanzisha kanuni za Sekta ya Posta ambapo TCRA imepewa jukumu la kusimamia utoaji wa huduma za Posta ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria ya TCRA inazuia ufanyaji wa shughuli za Posta bila ya leseni halali inayotolewa na TCRA, TCRA pia inahakikisha uwapo wa huduma za posta zenye kuaminika, usalama, ufanisi na bei nafuu ndani ya Jamhuri ya Tanzania.

Kwa muktadha huu,TCRA imeandaa mazingira ya kudhibiti utoaji wa huduma za Posta kwa kuandaa kanuni na nyenzo ambazo zitawezesha kufungua soko na kusaidia ubunifu katika utoaji wa huduma, hizi nyenzo za kudhibiti ni pamoja na Mfumo wa Leseni za Sekta ya Posta ambayo inatoa mwongozo wa utoaji leseni za posta nchini.

Utoaji wa Leseni za Posta

Mfumo wa Utoaji wa Leseni za huduma za Posta na zile za kusafirisha nyaraka, vifurushi na vipeto ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimegawanyika katika makundi sita ambayo ni:

  1. Leseni Mtoa huduma za msingi za Posta: Leseni hii inatolewa kwa Shirika La Posta Tanzania (TPC) kwa kipindi cha miaka ishirini na Tano (25) ambayo inahuhishwa baada ya muda kuisha.
  2. Leseni ya Kimataifa ya Mtoa Huduma Binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) kutoka /kwenda nje ya nchi. Muda wa leseni hii ni miaka mitano (5) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  3. Leseni ya Afrika Mashariki ya Mtoa Huduma Binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) kutoka /kwenda jumuiya ya Afrika Mashariki. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  4. Leseni ya Ndani ya nchi ya Mtoa Huduma Binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  5. Leseni ya Ndani ya mkoa mmoja nchini ya Mtoa huduma binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.
  6. Leseni ya kati ya vituo/mikoa miwili kwa msafirishaji nchini ya Mtoa huduma binafsi ya Posta: Leseni hii inatolewa kwa watoa huduma binafsi wa usafirishaji ambao wanapokea, wanakusanya na kusambaza bidhaa za Posta (Nyaraka, vifurushi na vipeto) kati ya vituo/ mikoa miwili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muda wa leseni hii ni miaka mitatu (3) na inaweza kuhuishwa baada ya muda kuisha.

Jedwali:: Ada za leseni za watoa huduma za Posta

Na. Kundi la Leseni Ada ya Maombi (Shs.) Ada ya Mwaka wa kwanza (Shs.) Ada ya Maombi ya Kuhuisha (Shs.) Ada ya Mwaka (Shs.)
1Mtoa Huduma za Posta za Msingi 2,300,00020,000,0002,300,00020,000,000
2 Mtoa Huduma za Kimataifa170,00018,000,000170,00018,000,000
3Mtoa Huduma ndani ya Afrika Mashariki 100,000 6,000,000 100,000 6,000,000
4 Mtoa Huduma za Binafsi wa Ndani ya Nchi 60,000 3,000,000 60,000 3,000,000
5Mtoa Huduma binafsi ndani ya Mkoa mmoja 60,000 1,400,000 60,000 1,400,000
6Mtoa Huduma Binafsi wa Posta kati ya Mkoa miwili 60,000 400,000 60,000 400,000

Unaweza kupakua kanuni za Mawasiliano ya Kielektroni na Posta kwa upande wa leseni kwa kubofya https://www.tcra.go.tz/documents/regulations

Kwa ajili ya kuomba leseni bofya https://tanzanite.tcra.go.tz/login.htm

Kwa kutoa maoni/malalamiko https://www.tcra.go.tz/pages/complaints