1. Ubia wa Kimkakati
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasimamia sekta wezeshi ambayo ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa kidijiti kwa kutoa leseni za huduma za mawasiliano na kufutilia ubora huduma zinazotolewa Vilevile inasimammia kanuni za mawasiliano zilizotungwa chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.
Mojawapo ya kanuni hizo inahimiza watoa huduma kuchangia matumizi na uendeshaji wa miundombinu, ambayo hutumika katika mifumo wezeshi ya Kidijiti na Uchumi wa Bluu.
Uchangiaji miundombinu, kama vile minara ya mawasiliano una faida za kiuchumi kwa watoa huduma, kwa kuwa wanapunguza gharama za ujejenzi wa miundombinu mipya na kunalinda mazingira. Kuchangia miundombinu hunufaisha wananchi kupitia ufanisi wa huduma ambapo jamii inanafikiwa na huduma inayo wawezesha kuingia kwenye mfumo jumuhishi wa Uchumi ikiwepo huduma za kifedha, elimu, biashara na zinginezo kwa Kuchangia miundombinu.
Maendeleo ya sekta ya mawasiiano Tanzania yamechangiwa na sera nzuri na mipango mizuri ya serikali, mfumo imara wa kisheria na kiusimamizi na pia mahitaji ya soko.
Serikali inatumia uwezo wa sekta binafsi katika ubunifu na ufanisi. Mifano ya hivi karibuni ni pamoja na kwenye utekelezaji wa mradi wa kujenga minara mipya maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto kibiashara, Tanzania Bara na Zanzibar ambapo Zaidi ya wananchi milioni 8.5 wamefikiwa na huduma.
2. Ukuaji na ueneaji wa kasi wa teknolojia na huduma
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema huduma kupitia teknolojia ya simu uzao wa tano, yaani 5G imefikia asilimia 34.18 ya watu Tanzania imeenea kwa zaidi ya asilimia 11 nchini kote. Hali hii inaonesha ukuaji wa kasi wa mtandao wa kasi (5G) tangu ulipoingia nchini mwaka 2022.
Teknolojia ya 5G ina kasi kubwa na bora zaidi; na inaweza kuunganisha watumiaji na vifaa vingi vya mawasiliano kwa wakati mmoja bila kupoteza ubora. Aidha, huduma kupitia uzao huu ni imara na uwezo mkubwa wa kusafirisha taarifa nyingi zaidi kwa wakati mmoja na kwa kazi zaidi. 5G pia hutumika kwenye viwanda na mitambo ya kisasa, kwa mfano Reli ya Kasi (SGR), mitambo ya uzarishaji mali, ndege nyuki (drone) katika kusafirisha mizigo na kumwagiria dawa kwenye mimea.
Mhandisi Mwasalyanda amesema, Mawimbi ya simu ya 2G yalienea asilimia 98.66 ya watu, 3G ilienea asilimia 93.95 ya watu, na 4G imeenea kwa 94.39 miongoni mwa watu. Mikoa yote Tanzania ina vifaa vya kuwezesha huduma za 5G, kwa 34.18 %.
3. Usalama wa Mtandao na Sera ya Faragha
Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Mawasiliano Duniani (ITU) Kitengo cha Usalama mtandaoni (Global Cyber Security Index (GSSI) imebainisha kwamba Tanzania, ni ya kwanza kwa uthabiti wa mifumo yake ya mtandao kati ya nchi za Afrika Masharaki na Kati.
Pia Tanzania ni mojawapo ya nchi 45 vinara, za mfano bora, zakuigwa duniani. Kanuni za huduma za mawasiliano zinalinda faragha za watumiaji wa huduma hizo kwa njia mbalimbali. Uthabiti katika huduma za mawasiliano nimuhimu katika kuwezesha wananchi kuwa na Imani na mifumo hiyo ambapo huweza kuitumia kwa uhuru na ufanisi kwasababu wanakuwa na Imani na mifumo husika.
TCRA imetoa namba fupi maalum kwa ajili ulinzi wa watumiaji wa huduma za mawasiliano. Kwa mfano, namba 15040 hutumika kuripoti namba za matapeli wanaofanya uhalifu mitandaoni. Namba 100 hutumika kwa ajili ya mawasiliano kati ya mtoa huduma na mtumiaji wa huduma za mawasiliano pekee. Msimbo *106# hutumika kuhakiki idadi ya laini za simu zilizosajiliwa kwa namba ya NIDA ya mtumiaji. Huduma zote hizi hazina malipo ni BURE.
4. Ubunifu na ujasiriamali wa Teknolojia
Sera ya Taifa ya teknolojia ya habari na mwasiliano (TEHAMA) ya mwaka 2016, ambayo imepitiwa upya na kurekebishwa, inatambua mchango wa mazingira wezeshi ya kisera na kiusimamizi kwenye kukuza uvumbuzi kidijitali.
Sera hiyo inalenga kuibadili Tanzania kuwa ya kidijiti, yenye uchumi imara ambao unawezesha na kuendeleza uvumbuzi na ujasiriamali wa kidijiti. Vilevile lengo ni kuwezesha Tanzania kufikia na kupita malengo ya kikanda Afrika na kimataifa kama yalivyoainishwa kwenye Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030 na yale ya Dira ya Umoja wa Afrika 2063.
Serikali, kupitia TCRA husaidia wabunifu ambao miradi yao inauwezo wa kutengeneza program za TEHAMA zenye uwezo wa kuleta ufumbuzi wa changamoto mbali mbali za Kijamii.
Kwa muktadha huu, TCRA inaendeleza uvumbuzi nchini kwa kutoa kwa vipindi maalum na bila malipo raslimali za mawasiliano kwa wavumbuzi na kampuni changa za mawasiliano kujaribu miradi yao. Raslimali hizo ni masafa, namba na misimbo, kikoa cha Tanzania na postikodi.
TCRA imechapisha mwongozo kwa watafiti, wavumbuzi, na waanzishaji katika kutuma maombi na kutumia rasilimali za mawasiliano ili kujaribu yao au uvumbuzi wao.
Azma ya TCRA ya kuwezesha ujenzi wa jamii ya Kitanzania kupitia matumizi ya huduma na bidhaa za mawasiliano.
Mpango huu umewezesha kampuni changa tano za Kitanzania kuibuka kidedea Afrika. Kampuni changa tano kati ya 10 zilizotambuliwa kwa umakini na Umoja wa Mawasiliano Afrika (ATU) mwaka 2025 ni za Tanzania.
ATU inatekeleza mpango wa kuendeleza uvumbuzi kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) Afrika ili kuharakisha mabadiliko ya kidijiti barani humu. Taasisi hiyo ni chombo cha Umoja wa Afrika (AU) kuhusu masuala ya TEHAMA.
5. Utoaji wa Huduma Kidijitali
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeweka ufanisi na kurahisisha utoaji wa huduma zake kwa kutumia mifumo ya kidiji ikiwemo Dawati la Huduma kwa Mteja na Tanzanite Portal.
Dawati la huduma kwa mteja, hufanya kazi Saa 24, Siku Saba kwa wiki, ambapo Wawekezaji kwenye sekta ya mawasiliano na wananchi mbalimbali wanahudumiwa kikamilifu sehemu waliko bila kufika ofisi za TCRA. Wateja wa TCRA wanaweza kutumia baruapepe: dawatiladuma@tcra.go.tz au wanaweza kupiga simu 0800008272 BURE.
Tanzanite Portal, nimfumo muhimu wezeshi ambao TCRA inatumia katika kuhudumia wananchi popote pale nchini, bila kufika ofisini. Mfumo huu huwezesha wawekezaji kuomba leseni, kufanya malipo na kupata leseni wakiwa popote pale nchini bila ya kufika ofisi za TCRA na bila kutumia lundo la karatasi. Watoa huduma za mawasiliano pia huweza kuhuwisha leseni zao, kufanya malipo na kupata taarifa za ziada kupitia mfumo wa Tanzanite, ambapo huduma hutolewa kwa kasi na ubora, bila kupoteza mda.
Pia Tovuti ya TCRA imekuwa nimoja ya tovuti ya kwanza hapa nchini, kuwa na Alama maalum zinazowawezesha watu kwenye mahitaji maalum (kama wenye uono hafifu, Usikivu hafifu ) kuitumia kupata huduma mbalimbali kutoka TCRA na kuwasilisha taarifa na kutoa maoni nao kwenda TCRA.
6. Ujuzi wa Kidijitali na Ajira -Klabu za Kidijiti
TCRA pia inahimiza uanzishaji wa klabu za kidijiti kwenye taasisi za elimu nchini kote kujenga kizazi chenye umahiri wa kidijitali. Klabu hizi ni za ihari ambapo TCRA pia husaidia wabunifu wachanga au wadogo (startups), kuanzia shule za awali, shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati hadi Chuo Kikuu kuja na masuluhisho ya kidijitali.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa TCRA kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya TEHAMA ambazo zinawezesha kutumia mifumo ya kidijitali na program wa TEHAMA katika ngazi zote za matumizi kwenye sekta mbalimbali.
Uanzishwaji wa klabu za kidijiti ni msingi mkuu wa kuwezesha ubunifu wa ndani Tanzania na uvumbuzi unaolenga kutatua changamoto zakijamii maeneo husika.
Hadi June 2026 vilabu vya kidijiti 800 vilikuwa vimeanzishwa kupitia miradi 70. Hivi vina wanafunzi wanachama 3,509 na walimu 885.
7. TCRA husimamia Ubora wa Huduma za Mawasiliano
TCRA huatilia na kusimamia ubora wa huduma za Mawasilinao ikitumia mitambo ya kisasa ambapo taarifa ya robo mwaka inayoishia Juni 2026 iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda imeonesha kuwa watoa huduma wote wanakidhi vigezo vya ubora vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ubora za mwaka 2018, ambapo hadi sasa ubora wa huduma zao ni Zaidi ya asilimia 90 kwa wastani. Ubora wa huduma ni pamoja na Usikivu wa uhakika na kutumia simu kuongea au intaneti kwa mda mrefu bila kukatika.
8. Maabara ya kisasa ya Vifaa vya Mawasiliano
TCRA imefanikiwa kujenga maabara bora na yakisasa zaidi barani Afrika kwa ajili ya Uidhinishaji wa vifaa vya Mawasiliano ambavyo hufanyika kwa modeli ya kifaa husika na hufanyika mara moja tu. Zoezi hili ni muhimu katika kuhakikisha kwamba vifaa vyote vinakidhi viwango vya usalama ili kuwalinda watumiaji na umma dhidi ya hatari zinazoweza kutokea, kama vile mionzi isiyo salama au miale hatarishi.
Vifaa hivyo nipamoja na Simu za Mkononi, Simu za mezani, Modemu za data, Redio za VHF/UHF, Rimoti, Kamera za Kidigitali, televisheni za smart, Visimbuzi, Mifumo ya Mawasiliano ya Ofisi na Vifaa vya Utangazaji ni baadhi ya vifaa vinavyoidhinishwa na TCRA ili kukidhi vigezo mbalimbali vya Kitaifa na Kimataifa katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa vifaa vya Mawasiliano.
Aidha watumiaji wa vifaa vya mawasiliano wanakumbushwa kutumia vifaa ambavyo vimeidhinishwa na TCRA, ili kulinda usalama wao na kupunguza uwezekano wa matatizo ya kifundi, kuharibika haraka kwa vifaa, au matatizo ya utendaji kazi ambayo yanaweza kusababisha usumbufu kwa watumiaji.
Uidhinishaji wa vifaa vya Mawasiliano hufanyika kwa modeli ya kifaa husika na hufanyika mara moja tu. Zoezi hili ni muhimu katika kuhakikisha kwamba vifaa vyote vinakidhi viwango vya usalama ili kuwalinda watumiaji na umma dhidi ya hatari zinazoweza kutokea, kama vile mionzi isiyo salama au miale hatarishi.





