TCRA

TCRA

Creating a Level Playing Field

Initializing...
Published13th Apr, 2021
Last Updated29th Apr, 2021
Read Time1 min

Termination of Restrictions on Service Providers to use Freelancers for Biometric Sim Card Registration

KUSITISHA ZUIO KWA WATOA HUDUMA KUWA TUMIA “FREELANCERS” KATIKA USAJILI WA LAINI ZA SIMU Ikumbukwe kuwa tarehe 16 Februari, 2021 baada ya kuwa na kikao na watoa huduma za Mawasiliano ya simu, TCRA iliwaelekeza watoa huduma kusitisha kuwatumia “Freelancers” katika usajili wa laini za simu kibayometria ifikapo 1 Mei, 20…

Share On
Termination of Restrictions on Service Providers to use Freelancers for Biometric Sim Card Registration

KUSITISHA ZUIO KWA WATOA HUDUMA KUWA TUMIA “FREELANCERS” KATIKA USAJILI WA LAINI ZA SIMU

Ikumbukwe kuwa tarehe 16 Februari, 2021 baada ya kuwa na kikao na watoa huduma za Mawasiliano ya simu, TCRA iliwaelekeza watoa huduma kusitisha kuwatumia “Freelancers” katika usajili wa laini za simu kibayometria ifikapo 1 Mei, 2021 na badala yake usajili ufanyike katika maduka au mahali maalum kwa mujibu wa Kanuni za Usajili wa laini za Simu za 2020. Napenda kuwajulisha kuwa TCRA imeondoa zuio hilo kwa watoa huduma na wanaweza kuendelea kuwatumia “Freelancers” bila kuathiri usajili sahihi wa laini za simu kibayometria wakati inafanya tathmini upya ya namna bora inayoweza kutumiwa na watoa huduma kuwa simamia “Freelancers”.

TCRA, inatoa rai kwa “Freelancers” kuhakikisha kuwa wanatumia weledi katika kufanya kazi yao ya usajiliwa laini za simu. TCRA itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu huduma za mawasiliano kwa ustawi na maendeleo ya Taifa.