Weledi:
Tunatekeleza majukumu yetu kwa kutoa huduma bora tukizingatia maadili na heshima kwa wateja wetu;
Utendaju wa Pamoja:
Tunaamini katika utendaji kazi wa pamoja ili kutatua matatizo na kutambua kwamba mawasiliano imara ni muhimu katika kujenga mazingira ya ushirikiano;
Ubunifu:
Tunazingatia ubunifu katika kushughulikia masuala ya kiudhibiti sanjari na mabadiliko ya teknolojia duniani;
Uwajibikaji:
Tunawajibika kikamilifu na kuchukua dhamana tunapotoa huduma;
Uadilifu:
Tunatekeleza kazi zetu kwa kuzingatia maadili, uthabiti na uaminifu wa hali ya juu.



