TCRA

TCRA

Creating a Level Playing Field

Initializing...

Wajibu, Kazi & Nguvu

Kuelewa mamlaka yetu ya kisheria na majukumu.

Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoianzisha TCRA inaipa Mamlaka wajibu katika majukumu yafuatayo:

1. Kukuza ushindani bora na uchumi wenye tija;

2. Kulinda maslahi ya watumiaji;

3. Kulinda mitaji ya Watoa Huduma wenye ufanisi;

4. Kukuza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa watumiaji wote wakiwamo wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji walio na walioko katika mazingira magumu;

5. Kuimarisha Elimu kwa Umma, uelewa na ufahamu wa huduma zinazosimamiwa na TCRA, ikiwa ni pamoja na:

(i) Haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazosimamiwa;

(ii) Namna ya kuwasilisha malalamiko na migogoro na utaratibu wa utatuzi wake; na

(iii) Kazi na majukumu ya Mamlaka kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira.