JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), inatambua na kuamini kwamba, mafanikio yake yanaambatana na wajibu wa kuisaidia jamii kwa utaratibu unaoeleweka na endelevu. 

TCRA ina mkakati unaolenga kuimarisha taswira na sifa ya taasisi. Mkakati huu unalenga kusaidia jukumu la uwajibikaji kwa jamii wenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kwa kupunguza umaskini na kukuza maendeleo ya kiuchumi kupitia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

TCRA imechagua maeneo ya vipaumbele ambavyo vitazingatiwa wakati wa kutoa misaada. Maeneo hayo mtambuka yapo sanjari na majukumu ya Mamlaka kuyafikia maeneo mbalimbali ya Tanzania. Maeneo haya ni pamoja na:
i. Maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano, na 
ii. Elimu

Maeneo hayo yanashabihiana na Vipaumbele vya Maendeleo ya Taifa. TCRA inashirikiana na washirika wa ndani na nje ya nchi au asasi za kijamii ili kukuza uwekezaji katika programu za maendeleo ya jamii zinazohusiana na masuala ya TEHAMA. Wakati wote, TCRA imejitolea kuhakikisha kuwa Uendelevu, Uwajibikaji na Uwazi vinazingatiwa vizuri. Mamlaka itawasiliana na jamii na wadau ili kukuza taswira na sifa ya taasisi.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!