JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
Dkt. Jabiri Kuwe Bakari
Mkurugenzi Mkuu

Wadau wetu!

Katika jitihada za kufanikisha dira yetu ya kuwa “Msimamizi wa Kiwango cha Kimataifa kwa Mawasiliano ya Elektroni na Posta”,  Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)(TCRA) inalenga kuimarisha uwezo wake wa kuhimiza ufikishwaji wa bidhaa na huduma za mawasiliano kwa kila mtu kwa kushughulikia kimkakati mazingira ya udhibiti wa mawasiliano ya elektroni na Posta yanayobadilika kwa kasi.

TCRA inalenga kujenga mazingira ya udhibiti ili kuboresha uchumi wa kidijiti unaochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Kutokana na mafanikio ambayo sekta ya mawasiliano imeyapata mpaka sasa, ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa ujumuishaji wa teknolojia ya kidijiti na Mtandao wa brodibendi unawafikia wananchi wengi .

TCRA imedhamiria kudumisha mazingira ya uwezeshaji yenye ushindani kwa uwekezaji wa sekta binafsi yanayochagiza upanuzi wa mtandao na huduma, mawanda ya ufikishwaji wa maudhui ya vyombo vya utangazaji na utengenezaji wa maudhui ya ndani. Aidha TCRA itaendelea kuboresha miundombinu muhimu ya huduma za Posta na usafirishaji wa vifurushi na vipeto na vifurushi kwa huduma za ki-elektroni na mifumo ya utumiaji.

Ili kutimiza Dhamira yetu, TCRA itaendelea kuimarisha uelewa wa watumiaji  kwa kutumia programu mbalimbali za uelimishaji si katika kutambua haki na wajibu wao bali pia kuwawezesha kufanya uamuzi sahihi wa huduma na bidhaa za mawasiliano wanazozihitaji.

Fauka na hayo, TCRA itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wake ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiwango cha juu cha uadilifu, weledi na uwajibikaji na kuhakikisha kuwa wana afya njema.

Mwisho, TCRA inaendelea na dhamira yake ya kutoa huduma bora za udhibiti kwa kuzingatia “udhibiti kwa mashauriano” kama njia ya kukuza na kutekeleza muundo wa udhibiti wenye kuleta tija.

Salamu,

MKURUGENZI MKUU

 

 

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!