JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

SERA YETU YA UBORA

Kutokana na nguvu za kisheria  za kusimamia sekta za Mawasiliano ya Kielektroni na Posta Tanzania, TCRA imejidhatiti kuweka mazingira mazuri kwa Wenye Leseni kwa kutoa rasilimali,  kudumisha na kuendelea kuboresha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ili  kuhakikisha utoaji wa huduma bora na nafuu kwa watumiaji ili kukidhi matakwa ya Sheria na ya kiudhibiti.

MALENGO YA UBORA (MWAKA 2022/2023)

1. Kuhakikisha Wenye Leseni wanakidhi viwango vya utoaji huduma bora ifikapo Juni 2023:

     a) Kuboresha upatikanaji wa Mtandao kutoka asilimia 99 hadi 99.9;
     b) Kuboresha ufikishwaji wa huduma za mawasiliano kama ifuatavyo: -
            i) Utangazaji wa Redio kutoka asilimia 40 hadi 60;
           ii) Utangazaji wa Televisheni.
                   Kwa mfumo wa setelaiti kutoka asilimia 98 hadi 99.
                   Kwa mfumo wa ardhini (DTT) kutoka asilimia 50 hadi 80;
          iii) Huduma za mawasiliano kwa njia ya sauti kutoka asilimia 91 hadi 93;
          iv) Data (Intaneti) kutoka asilimia 51 hadi 54.
      c) Huduma za Posta:
    Kukidhi viwango vya posta kutoka asilimia 73 hadi 78;
      d)  Utangazaji wa Redio na Televisheni:
          i) Uzingatiaji wa ratiba na maudhui ya vipindi kutoka asilimia 72 hadi 74;
         ii) Uzingatiaji wa mgawanyo wa vipindi vya ndani na nje kutoka asilimia 63 hadi 68.

2. Kuhakikisha gharama za jumla za ada inayotozwa kwa simu za sauti inasalia kuwa TSH 2.00 kwa Dakika ifikapo Juni 2023.

3.  Kuboresha kiwango cha kuridhika kwa watumiaji na watoa huduma za mawasiliano ifikapo Juni 2023 kwa:-

      a) Kupunguza muda wa kupata Leseni za mawasiliano (kwa wastani) kutoka siku 90 hadi 60;
      b) Kupunguza muda wa kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kutoka siku 60 hadi 55, kuanzia siku ya kusikilizwa kwa shauri;
      c)  Kuongeza kiwango cha ubora wa kuridhishwa na huduma kwa watumiaji wa huduma kama ifuatavyo: -
           i) Huduma za sauti: kutoka asilimia 94.8 hadi 95;
          ii) Huduma za intaneti: kutoka asilimia 83 hadi 95;
         iii) Huduma ya Fedha kupitia simu za mkononi: kutoka asilimia 79.5 hadi 95.

4. Kuboresha utamaduni wa Udhibiti kwa Mashauriano ifikapo Juni 2023 kwa: -

      a) Kupandisha Kiwango cha kuridhishwa cha ushirikiano na wadau kutoka asiliimia 92 hadi 93;
      b) Kuboresha kiwango cha uoanishaji wa mifumo ya kiudhibiti ya ndani na ile ya kikanda na kimataifa kutoka asilimia 67 hadi 71.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!