JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

TCRA inamtambua mmilki wa domeini kama kampuni au mtu binafsi iliyoweka/aliyewekwa kwenye kanzidata ya rajisi kama msajiliwa wa domeini wakati wa usajili wa domeini.



Iwapo kampuni au mtu binafsi inatumia/anatumia mtu mwingine au wakala kusajili majina ya domeini yake, sharti wahakikishe kwamba wameonyeshwa kama wanaosajiliwa kwa domeini husika na si vinginevyo.


Kwa kawaida ada za mwaka za domeini zinalipwa kila mwaka tarehe ambayo domeini ilisajilliwa. Iwapo ana za mwaka hazitalipwa, domeini itaingia ngazi ya kumalizika muda wake, ambapo taarifa itatumwa kwa mhusika wa kuendesha domeini na mwenye domeini aliyesajiliwa. Siku 30 baada ya ngazi ya domeini kumalizika muda, domeini itapelekwa kwenye ngazi ya Kutolewa, yaani Out-of-zone (OOZ), ambamo domeini itabakia kwenye kanzidata ya rajisi lakini haitapatikana kwenye mfumo wa DNS. Wakati domeini ikiingia kwenye ngazi ya OOZ, taarifa itatumwa wakati huo huo  kwa mhusika wa kuendesha domeini na mhusika wa masuala ya kiufundi. Domeini itabakia kwenye ngazi ya OOZ kwa siku 30 zaidi kabla haijafutwa. Baada ya kufutwa, domeini itaondolewa moja kwa moja kutoka kwenye kanzidata ya rajisi  na hapo hapo inapatikana kwa ajili ya usajili na mhusika mwingine anayesajiliwa. 


Mhusika wa masuala ya kiufundi anawajibika kwenye kuendesha na kusasisha kompyuta zinazohifadhi taarifa za Mfumo wa vikoa ambazo zinahusika na jina la domeini


Mhusika wa kuendesha domeini anaidhinishwa na yule anayesajiliwa kuwasiliana na rajisi (TCRA) au msajili wa majina ya domeini kujibu maswali kuhusu usajili wa majina ya domeini na anayesajiliwa.


Ndio; iwapo anayesajiliwa haridhiki na huduma za msajili aliye naye, yuko huru kuhamisha domeini zake kwa msajili mwingine wanayemtaka.



Utaratibu uliowekwa wa kuwasilliana na domeini unahitajika katika kuulizia na kufuatilia msimbo wa kuhamisha domeini kutoka kwenye rajisi, ama kwa kupitia sehemu ya tovuti ambamo mhusika anajihudumia mwenyewe kwenye tovuti ya https://karibu.tz  au kwa maandishi kwenda kwenye rajisi kupitia rajisi@tcra.go.tz.


Ufunguo wa Rajisi ya Jina la Domeini unajulikana pia kama Nywila ya Domeini. Ni nywila yenye msimbo uliochanganywa ambayo inakutruhusu kuhamisha Jina la Domeini kwenda kwa Msajili mwingine.


Ndiyo; kuanzia tarehe 1 Machi 2022, wanaosajiliwa wataruhusiwa kusajili domeini moja kwa moja chini ya domeini ya kiwango cha juu ya fumbo ya dot tz; kama vile karibu.tz. Domeini hizi zinajulikana kama domeini za kiwango cha juu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejea Mwongozo wa Usajili wa domeini za ngazi ya Pili ambao unapatikana:  https://karibu.tz/.


Ada za majina ya domeini zinapatikana kwenye kiambatanisho cha pili cha Kanuni za Mawasiliano ya Kielektoniki na Posta (Usimamizi wa Majina ya Domeini) za 2020. Ili kuunganishwa na kuona bofya: https://karibu.tz/media/regulations.pdf


Orodha ya wasajili walioidhinishwa inapatikana kwenye kwenye tovuti ya Karibu. Ili kuunganishwa na kuona orodha, bofya kwenye: https://karibu.tz/domains/registrars/


Unaweza kusajili majina ya domeini kwa kuchagua mmojawapo wa wasajili walioidhinishwa na ambao wamechaoishwa kwenye sehemu iliyoko kwenye tovuti ya Karibu. Ili kuunganishwa na kuona orodha, bofya kwenye:. https://karibu.tz/domains/packages/


Majina ya Domeini ya ya Fumbo  ngazi ya Pili ni kama ifuatavyo:




  1. <jina>.co.tz –  kwa taasisi yoyote, ikiwa ni pamoja na kampuni au biashara zilizosajiliwa;

  2. <jina>.or.tz –  taasisi zisizojiendesha kibiashara;

  3. <jina>.go.tz –  domeini iliyotengwa kwa taasisi za Serikali ya Tanzania kama zinavyotambuliwa kupitia Bunge au kwa kuwa na barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara husika ilipo taasisi hiyo;

  4. <jina>.ac.tz– domeini iliyotengwa kwa vyuo vya elimu au taasisi za ufundi zenye usajili kama ipasavyo;

  5. <jina>.ne.tz – kwa mtandao wa watu au bidhaa;

  6. <jina>. mil.tz – domeini iliyotengwa kwa taasisi za kijeshi za Tanzania zinazotambuliwa na Wizara yenye majukumu ya  Ulinzi.

  7. <jina>.sc.tz – domeini iliyotengwa kwa shule za awali, msingi na taasisi za ngazi ya sekondari;

  8. <jina>. info.tz – kwa domeini zinazotoa habari kuhusu masuala mahsusi;;

  9. <jina>.tv.tz – kwa matumizi ya watunza maudhui, watengenezaji wa filamu na stesheni za televisheni;

  10. <jina>. mobi.tz – kwa watoa huduma kupitia vifaa vya mkononi;

  11. <jina>. hotel.tz – kwa watoa huduma za malazi na ukarimu; na

  12. <jina>.me.tz – kwa watu binafsi.


Meneja (ccTLD) ni taasisi (kampuni) au mtu binafsi ambaye anashughulikia masuala ya kila siku ya Domeini ya Kiwango cha juu ya Fumbo au shughuli zinazoambatana nayo kwa niaba ya jumuiya ya intaneti alipo.



Mamlaka inayokasimu majukumu kwa Meneja wa Domeini ya Kiwango cha juu ya Fumbo ni taasisi ya kimataifa inayosimamia masuala ya intaneti, inayoitwa  ICANN, ambacho ni kifupisho cha  Internet Corporation for Assigned Names and Numbers.



Kwa kikoa cha dot tz (.tz) cha  ccTLD, meneja ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.


Huyu ni taasisi au mtumiaji binafsi ambaye anasajili kikoa. 


Ni mtu au taasisi iliyopewa kibali na Mamlaka kusajili, kufuta, kuongeza, kurekebisha au kubadili vikoa chini ya utaratibu wa vikoa vya dot tz (.tz).


Rajisi inafanya kazi kama hazina ya yenye mamlaka inayohifadhi taarifa zote zinazotakiwa kutoa ufumbuzi wa vikoa vilivyosajiliwa kwenye domeini ya kiwango cha juu ya fumbo (TLD) na rajisi hiyo au domeini za ngazi ya pili (SLDs) iwapo mfumo wa SLD unatumika (kwa mfano co.tz, ac.tz).



Rajisi hiyo pia inaweka taarifa za ziada kama vile uendeshaji wake na utaratibu wa kiufundi wa kuwasiliana nayo, namna ya kuwasiliana na domeini husika, utaratibu wa mawasiliano kwa ajili ya ankara na mrajisi aliyesajili kikoa hicho.


Domeini ya Kiwango cha Juu ya Fumbo la Nchi, (kwa ufupi ccTLD) ni domeini ya kiwango cha juu ya fumbo ambacho kawaida kinatumika au kimetengwa kwa nchi, dola  huru au eneo la nchi linalotambulika kwa msimbo wa nchi.



Domeini ya kiwango cha juu ya fumbo ina urefu wa herufi mbili; kwa mfano TZ ni Tanzania, KE ni Kenya, UK ni Uingereza.


Kwa lugha nyepesi, mfumo wa vikoa, au DNS in kitabu cha namba za mawasiliano kwa intaneti, unaounganisha watumiaji wa mtandao wa intaneti na tovuti mballimbali.



Mfumo wa vikoa, yaani DNS ni kanzidata iliyojengeka na duniani na ambayo inawezesha mawasiliano kupitia intaneti kwa kutafsiri majina haya ambayo ni rahisi kutumia (vikoa) kuwa misimbo mifupi ya namba (anwani za intaneti) ambazo kompyuta au vifaa  vinavyotumika kwenye mtandao vitazielewa; na kinyume chake.


Ni jina mahsusi linalotambua raslimali za intaneti kama vile tovuti zilizosajiliwa nchini na ngazi nyingine duniani.



 



Kompyuta zilizounganishwa kwenye intaneti zina anwani za namba mahsusi zinazoziwezesha kufikisha taarifa za kielektroniki mahali sahihi. Mfumo wa Majina ya domeini (DNS) unatafsiri anwani hizo za namba kwenye kompyuta na kuzipa majina ambayo ni rahisi kutumiwa. Vikoa vinavyojitokeza ni rahisi kukumbuka na vinasaidia watu kupata taarifa kwenye intaneti.



 Vikoa vinatumika kutambua kurasa mahsusi za tovuti. Kwa mfano, katika anwani ya tovuti ya "https://www.tcra.go.tz," kikoa ni tcra.go.tz.



 Vikoa pia vinatumiwa katika anwani za barua pepe ambazo zinawezesha watu kutuma na kupokea ujumbe wa kielektroniki; kwa mfano, barua@tcra.go.tz.


Piga simu dawati la huduma, namba 0800008272 au tuma barua pepe kwenda:  nms@tcra.go.tz.


Kwa sasa, huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu imesimamishwa kwa muda ili kuwezesha kuwa na mfumo mpya wa kuusimamia. Inategemea kurejea mwezi Juni, 2022.


Huduma ya mtumiaji kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba yake ya simu, yaani kwa kifupi MNP inakuwezesha kubakia na namba yako ya simu ya mkononi iwapo utaamua kubadili mtoa huduma za simu za mkononi Tanzania. Kimsingi; inakuwezesha kuendelea kutumia namba yako ya simu ya mkononi hata unapohamia mtandao mwingine. Kwa hiyo iwapo utabadili mtoa huduma za simu za mkononi, namba yako itabakia ile ile na hutahitajika kusumbuka kuwataarifu marafiki/familia/jamaa zako kuhusu mabadiliko ya mtoa huduma.


Ndani ya siku 14 za kazi.


Ada zote za raslimali za namba za mawasiliano zimeainishwa katika mwongozo kwenye tovuti ya Mfumo wa Usimamizi wa Namba, ambayo ni:  https://nms.tcra.go.tz:32443/nms/auvit/Application_Guidelines_and_Fees_for_Numbering_Resources.pdf


Ufuatao ni utaratibu wa kuomba raslimali za namba kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Namba, yaani NMS:



i. Fungua akaunti kwa kujisajili kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Namba.



2. Jaza wasifu wa Kampuni/Taasisi na ambatanisha nyaraka husika kama vile nakala iliyoidhinishwa ya Cheti cha usajili wa kampuni, Namba ya Mlipa Kodi na Katiba ya Kampuni.



3.Endelea na kujaza fomu ya maombi kwa kuchagua kipengele kinachohusika (mfano, Mpya, Kuongeza muda au Kubatilisha Maombi).



4. Kamilisha fomu ya maombi mtandaoni na wasilisha, kisha fuata maelekezo kutoka NMS kupitia taarifa zitakazotumwa kwako kuitia barua pepe uliyoiweka.


Hapana; ni lazima muombaje awe kampuni, Asasi isiyo ya Kiserikali, Taasisi ya Serikali au mwenye leseni ya Huduma za Programu Tumizi kutoka TCRA.


Yeyote mwenye leseni ya Mawasiiano ya Kielektroniki (mfano wenye mitandao ya mawasiliano ya simu za mkononi) au hata wengine kama vile Kampuni, Taasisi ya Serikali na Asasi zisizo za Kiserikali  (NGOs).


Mfumo wa Usimamizi wa Namba unafikiwa kupitia tovti ya TCRA ambayo ni: https://www.tcra.go.tz/   au moja kwa moja kwenye:  https://nms.tcra.go.tz:32443/nms/


Maombi yote ya raslimali za namba za mawasiliano yanafanyika mtandaoni kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Namba, yaani Numbering Management System au kwa kifupi NMS, ambao unapatikana kwenye tovuti ya TCRA, ambayo ni: https://www.tcra.go.tz/



  1. Kutoa majina na anwani, yaani kufikisha simu na ujumbe kwa mtumiaji husika au mahali husika ndani ya mtandao;

  2. Kuwapatia wanaopiga simu mwekeleo wa gharama zitakazotumika katika kupiga simu kwenye namba husika; mfano taarifa zinazoelezea kikamilifu eneo la kijiografia na gharama za kupiga simu kwenye mtandao wa mtumiaji na nje ya mtandao wake.

  3. Zinawawezesha watoa huduma kupanga viwango vya kutoza kwa mtumiaji mmojammoja au vya jumla (yaani gharama za maunganisho ya simu kati ya mitandao).

  4. Kuweza kufuatilia simu zinazopigwa, kutambua simu zenye malengo maovu, kuzuia na kutambua ulaghai.

  5. Kuweka na kutambulisha aina za huduma (mfano huduma na taarifa  vinavyotolewa bila malipo) na watoa huduma na mitandao mahsusi.


Namba ni raslimali muhimu katika utoaji wa huduma kwa watumiaji na katika kuendeleza ushindani na ubunifu katika huduma za mawasiliano ya simu. Watoa huduma za mitandao wanahitaji namba ili kutoa huduma za mawasiliano ya sim kwa watumiaji. Huduma hizo ni pamoja na:




  1. Simu za mezani;

  2. Simu za mkononi;

  3. Hduma za mawasiliano ya simu kupitia intaneti;

  4. Misimbo mifupi, ikiwa ni pamoja na ile inayotumika kwenye huduma za dharura (mfano 112 ya polisi) na huduma kwa wateja (mfano 100);

  5. Huduma za ziada za taarifa, huduma za kifedha na huduma za serikali;

  6. Premium Rates Services (PRS);

  7. Namba za bure (zisizolipiwa); na

  8. Mawasiliano kati ya mashine na vifaa vilivyounganishwa kwenye intaneti


Tovuti ya TZ-CERT, ambayo ni https://www.tzcert.go.tz/ inatoa taarifa kwa watumiaji wote na wasimamizi wa mifumo kuhusu tahadhari za usalama, ushauri, matangazo, miongozo na namna bora ya kushughulikia matatizo ya usalama.


Unaweza kupata kwa wakati taarifa za hivi karibuni kuhusu usalama kwa kujisajili ili kupata nakala ya jarida la TZ-CERT linalopatikana mtandaoni kupitia: https://www.tzcert.go.tz/subscribe-to-our-newsletter/.


Wakati wa kutoa taarifa ya tukio, ni muhimmu sana kutoa taarifa zilizo kamilika na kwa kina. Zinaweza kuwa na mambo yaliyoorodheshwa hapa chini au zaidi




  1. Jina la anayetoa taarifa na namna atakavyopatikana (mfano namba ya simu, anwani ya baruapepe).

  2. Namba inayoonyesha aina ya kifaa, namba ya kifaa, jina la anayehudumia tovuti ambao kifaa kimeunganishwa, anwani ya intaneti kama inaweza kufikiwa na watu wengi) na mahali ilipo.

  3. Tarehe na muda wa tukio.

  4. Maelezo ya kina kuhusu jambo lililotokea, ikiwa ni pamoja na namna kompyuta husika ilivyoshghulikiwa baada ya kugunguliwa tukio la kuwepo kirusi. Maelezo haya yawe kamili, yakiwa na nukuu ya maneno halisi yaliyoonyeshwa kwenye ujumbe wa tahadhari uliojitokeza kutoka kwenye programu ndogo ya malware au antivirus.


Taarifa ya tukio inaweza kutolewa kwa njia hizi:




  1. Kujaza kikamilifu na kuwasilisha fomu inayopatikana mtandaoni kwenye tovuti ya  TZ-CERT Website ambayo ni:



https://www.tzcert.go.tz/home/report-incidents-phishing-malware-or-vulnerabilities/




  1. Kutuma barua pepe kwenda:





PGP Key id: EED630F6



PGP Fingerprint: 0A1C CF48 D623 9BE7 676B 4C03 EF91 6FCA EED6 30F6


Tukio la kimtandao ni kitu kimoja au mfululizo wa vitu visivyotakiwa na visivyotarajiwa ambavyo vina uwezekano mkubwa wa kuathiri shughuli na utendaji au kutiia usalama wa taarifa, ambapo “Usalama wa Taarifa” ni kuhifadhi Usiri, Uimara na Upatikanaji wa Taarifa.


TZ-CERT inatoa huduma zilizoorodheshwa hapa chini bila malipo yoyote kwa wadau wake na umma kwa ujumla:




  1. Kutoa tahadhari, Onyo na Matangazo

  2. Kuchukua hatua dhidi ya matukio

  3. Kutoa elimu kuhusu uelewa wa masuala ya usalama mtandaoni

  4. Kutathmini udhaifu wa mifumo na kufanya majaribio ya kuingilia mifumo

  5. Kuchambua Ushahidi wa kidijitali kuhusu mifumo


TZ-CERT kifupisho cha kiingereza cha Kitengo cha Dharura cha Kitaifa cha Kushughulikia Masuala ya Usalama wa Mitandao.  Ni timu ya kitaifa yenye majukumu ya kuratibu matukio ya usalama katika mitandao kwenye ngazi ya  taifa na kushirikliana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa vinavyojihusisha na kusimamia matukio ya usalama mitandaoni.


Serikali imeweka Sheria na Kamati ya Maudhui yenye jukumu la kufuatilia maudhui ya Utangazaji yakiwemo maudhui ya wenye leseni za maudhui mtandaoni.



Kamati ya Maudhui hubainisha makosa katika maudhui ya utangazaji na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.  Pia, maudhui yenye sura ya jinai hufuatiliwa na kupepelezwa na Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Makosa ya Mtandao na kwa kutumia Sheria ya Makosa Mtandaoni. Jeshi la Polisi limekuwa likichukua hatua kwa watumiaji huduma za Mawasiliano wanaobainika kutumia isivyo huduma za Mawasiliano.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania-TAKUKURU ni taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kupambana na rushwa. Hivyo mwananchi anapaswa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa Taasisi husika ili kudhibiti vitendo vya rushwa.


TCRA tayari imeboresha na kuhuisha Kanuni za Utangazaji, ambapo gharama za leseni kadhaa zimefutwa na nyingine kupunguzwa.  Masuala ya kodi zinazosimamiwa na Mamlaka nyingine za kikodi, hushughulikiwa na Mamlaka husika.


Hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa na mtumiaji katika kusajili laini ya simu kwa njia ya biometria.


Unaweza kuthibitisha kuwa umesajiliwa kikamilifu kwa kupiga *106#.


Lengo la usajili kwa kutumia mfumo wa biometria ni kuimarisha usalama katika matumizi ya simu za mkononi, kulinda watumiaji na kufanikisha shughuli zingine za usimamizi wa sekta ya mawasiliano.


Mteja anatakiwa kufuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko. Kwanza, wasilisha malalamiko yako kwa mtoa huduma wako, endapo malalamiko hayatashughulikiwa au kusuluhishwa wasilisha malalamiko hayo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).


Fedha za mtu aliyefariki zilizopo kwenye akaunti au simu yake hupatikana kwa kufuata utaratibu wa mirathi kama ilivyo kwenye mali nyingine. Hivyo basi mtu aliyeteuliwa kusimamia mirathi anajukumu la kuchunguza na kukusanya mali zote za marehemu ikiwa ni pamoja na fedha za zilizopo kwenye simu yake ya mkononi au kwenye akaunti za benki.


Malalamiko yanye sura ya Jinai Kisheria yanashugulikiwa na Jeshi la Polisi Tanzania. TCRA inashauri ufungue Kesi Polisi ili suala lako liweze kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Malalamiko yanye sura ya Jinai Kisheria yanashugulikiwa na Jeshi la Polisi Tanzania. TCRA inashauri ufungue Kesi Polisi ili suala lako liweze kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inakufahamisha kuwa michezo yote ya bahatisha husimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania GBT). Hivyo inakushauri uwasiliane na GBT kwa kutumia namba 0800110051 (bila malipo) kwa  msaada zaidi na utatuzi wa lalamiko lako.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inakushauriwa kupata ripoti ya upotevu (lose report) kutoka Jeshi la Polisi yenye taarifa kamili ya kifaa chako ikiwa ni pamoja na namba tambulishi (IMEI) yake na uthibitisho wowote mwingine kuonyesha umiliki wa simu husika, kisha nenda kwa Mtoa Huduma wako wa SIM card liyokuwa ndani ya simu kabla ya kuibwa na kisha uombe kufunga simu husika. 



Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inakufahamisha kuwa masuala yote ya kijinai yanashughulikiwa na Jeshi la Polisi. Unashauriwa kuripoti kituo cha polisi kupata RB na Mpelelezi kwa ajili ya hatua stahiki. Kukiwa na kikwazo chochote ongea na Mkuu wa kituo au ngazi zinazofuata mpaka upate suluhisho.



Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.


Tanzania Communications Regulatory (TCRA) would like to inform that all issues related to fraud including fraud that is conducted through telecommunication is resolved by Police. TCRA advises a person who has encountered fraud to report the incident to Police station in order for Police to register the incident by providing an RB number and additionally, Police to assign an investigator who will be responsible for investigating the matter.



 Additionally TCRA would like to inform all who encounter fraud when using telecommunication services are advised to report the telephone numbers involved in fraud by writing SMS with keyword “UTAPELI” to number 15040. After sending the keyword to 15040 a notification will appear requesting to enter the phone numbers that were involved in fraud and here a subscriber should enter the phone number that were involved in the fraud incident that he/she encountered.



For more information or clarification consumers can contact TCRA by toll free number 0800008272 or by email- dawatilahuduma@tcra.go.tz


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, inakufahamishwa kuwa masuala yote kuhusu huduma za miamala ya kifedha, na husimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Unashauriwa uwasiliane na BOT kwa kupitia namba 022 223 4494-97 ulizia Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa (NPS) kwa ajili ya muongozo sahihi na kwa haraka. Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au kwa kuandika baruapepe dawatilahuduma@tcra.go.tz.



Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.


Wasilisha lalamiko lako kwa Mtoa Huduma wako kwa njia ya maandishi aidha kwa barua au baruapepe na pale usipo pata jibu ndani ya siku 30 au ukipata jibu usiloridhika nalo. Unapaswa kuwasilisha lalamiko lako TCRA na viambatanisho vya ushahidi wa kuwasilisha lalamiko lako kwa Mtoa Huduma wako. Kwa maelezo zaidi tupigie simu kupitia namba 0800008272 (bila malipo).



Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.


Kufanya utapeli mtandaoni ni kutenda kosa la jinai. Kosa la jinai ni tendo lolote ambalo limekatazwa kwa Sheria ambapo mtu yeyote akilitenda anakuwa ameikosea Jamhuri. TCRA hushirikiana na Jeshi la polisi kuhakikisha watu wanaojihusisha na utapeli mtandaoni wanabainishwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.


TCRA inahusika moja kwa moja katika kudhibiti Watoa Huduma za Mawasiliano nchini.


Zipo sababu nyingi ambazo husababisha vifurushi vya Mawasiliano kuisha ghafla au haraka kabla ya muda uliobainishwa. Miongoni mwa sababu ni uwezo wa simu janja unayotumia, mathalani kama ni simu ya kisasa, yenye uwezo mkubwa na kasi ya juu.  Pia, kutozifunga aplikesheni ambazo umezitumia, kuacha wazi kitufe cha ‘location’, na kuacha wazi kitufe cha roaming. Sababu nyingine ni kuongezeka kwa kasi ya internet, na kuwa na aplikesheni nyingi kwenye simu. Kiwango cha matumizi ya data kinategemea sana udhibiti wa mtumiaji wa kifaa cha Mawasiliano kiganjani; iwapo utahisi.


Kuhujumu miundombinu ya mawasiliano ni kutenda kosa la jinai. Kosa la jinai ni tendo lolote ambalo limekatazwa kwa Sheria ambapo mtu yeyote akilitenda anakuwa ameikosea Jamhuri. TCRA hushirikiana na vyombo vya dola vyenye jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria, likiwemo Jeshi la Polisi ilikuchunguza,kukamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wanaobainika kuhujumu miundombinu ya mawasiliano. Hivyo, ni wajibu wa kila mwananchi, kulinda miundombinu ya mawasiliano na kujiepusha na matendo ya jinai dhidi ya miundombinu ya mawasiliano.



  1. Unatoa njia muafaka na rahisi kwa Serikali na taasisi zake kuwasiliana na mwananchi kwa makusudi mbalimbali.

  2. Mfumo utarahisisha ufanyaji biashara ikiwa ni pamoja na za mtandao kwa wawekezaji wadogo hata wakubwa kwa vile biashara zitajulikana ziliko.

  3. Uandikishaji wa mali kama magari, biashara,wapiga kura utakuwa wa uhakika zaidi

  4. Njia rahisi ya kufanya utafiti kama sensa, sampuli za savei nk.

  5. Kuongeza utalii. Watapanga safari zao kuja nchini kwa ubora zaidi.

  6. Ufanisi katika shuguli za uokoaji majanga ya moto, magonjwa ya mlipuko, maafuriko na ajali.

  7. Itaongeza ubunifu kaatika matumizi ya intaneti na TEHAMA kwa ajili ya kutengeneza programu za kuongoza magari (GPS) na kusanifu ramani zinazotumika.


Mamlaka za Serikali za Mtaa ndizo zenye jukumu la kugawa na kusajili anwani wa wananchi wa eneo husika. Kwanza mtaa au barabara anayoishi mwananchi hutambuliwa na kuwekewa nguzo kuwa ina jina gani. Anwani ya makazi inagawiwa kwa mwananchi mwenye nyumba yake ambapo nyumba inapewa namba kutokana na barabara au mtaa ilipo. Aidha mlango wa mbele ya nyumba ndipo nambari ya nyumba itabandikwa upande wa kulia wa mlango ili ionekane.


Ndugu Lwitiko Ambele



4 Mtaa wa Mwakaleli



53122 Mwakibete



MBEYA


Postikodi pia hujulikana kama PIN Code nchini India,ZIP Code nchini Marekani, Postikodi nchini Canada na NPA katika nchi ya Uswizi inayoongea Kifaransa)




  1. Postikodi ni namba ya kiposta ambayo hutumika kutambulisha kwa usahihi eneo la utawala ambalo wananchi wanaishi.

  2. Postikodi ikitumika kwenye anwani humtambulisha mwananchi alipo kwa usahihi zaidi.

  3. Postikodi ni kitu chenye thamani katika nchi (rasilimali) na hutumika na wadau wengi kurahisisha shughuli za kibiashara.


Jukumu la kusajili namba za nyumba ni la Mamlaka za Serikali za   Mitaa. Namba za nyumba zitawekwa kwa mfumo ufuatao:-




  1. Kuanzia mwanzo wa mtaa upande wa kushoto itaanza nambari 1 na kulia nambari 2;

  2. Kwenye mduara namba zitazunguka kuanzia kushoto kwenda kulia;

  3. Sehemu zisizopangwa namba zitafuata mitaa kwa tafisiri ya Tawala za Mikoa.



  1. Mfumo wa anwani kwa kutumia nambari za nyumba, jina la mtaa au barabara na postikodi. Kwa mfumo huu anwani inatolewa kwa kila mwananchi

  2. Mpango huu unahusu utambuzi na uwekaji wa majina ya mitaa, barabara na namba za nyumba.

  3. Lengo kuu: Kutoa anwani ya uhakika kwa kila kaya na sehemu za biashara au huduma nchini kote ili kumfikia mwenye anwani kwa uhakika zaidi.


Ada za Idhini ya Vifaa  zinaweza kupatikana ukurasa wa 11 wa mwongozo wa Idhini ya vifaa ambao uko kwenye  https://otas.tcra.go.tz/downloads/Type_Approval_Guidelines.pdf.


Idhini ya vifaa inahitajika kwa antena ambazo zinaweza kuwashwa kielektroniki. Idhini ya Vifaa haihitajiki kwa antena ambazo haziwashwi.


Vifaa vinavyopokea tu mawimbi vinahitaji Idhini; kwa mfano vifaa vya kufuatilia mwenendo na mahali na vifaa vya kupokea mawimbi ya utangazaji


Cheti cha Idhini ya Kifaa hakiwezi kutolewa kwa aina nyingi za kifaa. Cheti hicho kinatolewa kwa msingi wa kila aina ya kifaa.


Cheti cha Idhini ya Vifaa kinachukuliwa kwamba wakati wote hakijamaliza muda wake iwapo hakuna mabadiliko yatakayofanywa kwenye kifaa kilichoidinishwa. Kifaa kinaidhinishwa mara moja tu lakini mtengenezaji au msambazaji anatakiwa kuitaarifu Mamlaka pale yanapotokea mabadiliko yanayoweza kuleta utofauti wa taarifa zilizohifadhiwa kwenye kanzidata ya Idhini ya Vifaa


Inachukua muda usiozidi siku 14 za kazi kutoa Cheti cha Idhini ya Vifaa kuanzia siku mwombaji atakapowasilisha nyaraka zote zinazohitajika na kama hapatakuwa na ucheleweshaji wa  malipo na kuwasilisha sampuni ya kifaa husika (pale  ambapo sampuni inahitajika kwa mujibu wa utaratibu wa maombi).


Muombaji wa Idhini ya Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki atawasilisha maombi yake kupitia mfumo wa mtandaoni wa maombi ya idhini ya vifaa, yaani OTAS, kifupisho cha Online Type Approval System ambao unapatikana kwenye https://otas.tcra.go.tz, ambamo mwombaji anaweza pia kupata taarifa za ziada.


Idhini ya vifaa inatakiwa ipatikane kabla kifaa husika hakijaingia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Watengenezaji wa vifaa na wawakilishi wao, kampuni za ndani na nje ya nchi zilizoidhinishwa, waagizaji au wasambazaji wa ndani wanaweza kuomba idhini kwa aina mpya ya vifaa vya mawasiliano vinavyokusudiwa kutumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kwa ujumla, Idhini ya Vifaa inatakiwa kwa vifaa vyote vya mawasiliano ya kielektroniki (vinavyotumia waya na visivyotumia waya) kabla ya kuingia soko la Tanzania. Mifano ya vifaa vinavyohitaji kuidhinishwa ni:



a) Vifaa vinavyotumiwa na wanaopata huduma za mawasiliano ya kielektroniki kama vile simu za mkononi, vishkwambi, simu za kawida, simu zisizo na waya, mod, redio za mawasiliano zinazotumia masafa ya VHF/UHF, Vifaa visivyotumia waya, kompyuta mpakato, skana, mashine ya faksi,vifaa vinavyoweza kusafirisha umbali mrefu taarifa zilizohifadhiwa kwenye kompyuta, ikiwa ni pamoja na vinavyowezesha kufuatilia na kutambua mwelekeo na mahali (GPS tracking devices), vifaa vya mawasiliano ya karibu, vifaa vinavyowasiliana kati yao kupitia intaneti na vifaa vya mawasiliano vyenye uweo mkubwa.



b) Vifaa vya mawasiliano ofisini kama vile mifumo inayosimamia usambazaji wa simu za ndani (PABX).



c) Vifaa vya mawasiliano mtandaoni kama vile vifaa vya swichi, vifaa kwenye minara ya mawasiliano, vifaa vya kuunganisha watumiaji wa intaneti, kompyuta za uwezo mkubwa  zinazohifadhi taarifa na vifaa vya kusambaza mawasiliano.



d) Vifaa vya utangazaji kama vile transmita,  vifaa vya mawasiliano kati ya studio na transmita, televisheni zenye uwezo mkubwa, visimbuzi, redio za kidijitali na amplifaya


Lengo la uidhinishaji wa vifaa ni kuhakikisha kwamba vifaa vyote vya mawasiliano ya kielektroniki vinakidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.



Vilevile, ni kuzuia madhara yoyote au athari zozote za kiafya kwa watumiaji, kuhakikisha usalama wa watumiaji na mazingira, kuzuia uwezekano wa vifaa hivyo kuingilia na kuharibu mitandao ya mawasiliano ya simu na kuimarisha ubora wa huduma za mawasiliano


Uidhinishaji wa Vifaa ni njia ya kuhakiki utengamano na muingiliano wa vifaa vyote vya mawasiliano ya kielektroniki na mtandao wowote wa mawasiliano ya kielektroniki na iwapo vinakidhi viwango.


EMF "ElectroMagnetic Fields" ni dhana inayohusiana na sumaku-umeme. Vifaa vyote vya umeme au elektroniki vinazalisha sumaku-umeme. Vyanzo vya kawaida vya EMF ni pamoja na kompyuta, televisheni, ovena za maikrowevu, vifaa visivyotumia waya kama simu za mkononi na vifaa vya Wi-Fi, laini za umeme, mifumo ya waya katika majumba,  paneli za umeme, transfoma, mota na aina zote za mifumo ya utangazaji, ikiwa ni pamoja na redio za AM na FM.



Pia, masafa na mifumo ya mwanga ya kawaida ni aina za EMF. Mbali na mwanga wa kawaida unaoonekana, aina nyingine za mwanga zisizoonekana kama vile mialekundu (infrared), na Urujuanimno (ultraviolet), eksrei na mionzi ya gamma ni aina za EMF.


Masafa ya redio, yanayofahamika pia kama “Radio Frequency – RF,” ni aina ya nishati ya sumaku-umeme inayozalishwa kwa kutumia Masafa ya juu kupitia vifaa vikubwa visivyohitaji muunganisho wa waya ili kuwezesha usafirishaji wa data.



Vyanzo vikuu vya RF ni pamoja na: miundombinu ya kurusha mawimbi ya masafa na televisheni, minara na antena za simu, simu zinazobebeka, simu za mkononi, mitandao ya kompyuta isiyo na waya (WLAN), na vifaa vya rada. Aidha, mifumo ya mawasiliano isiyo na waya inayotumika majumbani na kwenye majengo mbalimbali pia ni vyanzo vya RF.


RF EMF yaani "Radiofrequency Electromagnetic Fields" ni istilahi inayotumika kufafanua kiwango cha sumaku-umeme kinachojumuisha masafa kuanzia wigo wa kilohertz 100 (kHz) hadi Gigahertz 300 (GHz). RF EMF hutumika katika teknolojia mbalimbali, zaidi kwa madhumuni ya mawasiliano (kwa mfano simu za mkononi, vituo vya ubadilishanaji mawasiliano, Wi-Fi, 5G, redio, Luninga, vifaa vya usalama).



RF EMF pia hutumika katika tiba (kwa mfano mashine za uchunguzi wa afya za MRI), vifaa vya kupasha joto chakula (kwa mfano maikrowevu) na vifaa vya uhamishaji wa nishati bila waya (kwa mfano Qi).


Nchi mbalimbali huweka viwango vyao vya kitaifa vya mionzi (exposure) vinavyohusiana na sumaku-umeme.



Hata hivyo, sehemu kubwa ya viwango hivyo hutegemea miongozo iliyowekwa na Tume ya Kimataifa ya Ulinzi dhidi ya Mionzi isiyokuwa ya Ionizi (ICNIRP). Shirika hili lisilo la kiserikali, lenye uhusiano rasmi na Shirika la Afya Duniani (WHO), hufanya tathmini ya matokeo ya kisayansi kutoka nchi mbalimbali duniani. Kwa kuzingatia msingi wa mapitio ya kina ya maandiko ya utafiti, ICNIRP huandaa miongozo inayopendekeza viwango salama vya mionzi wa sumaku-umeme.



Miongozo hii hupitiwa mara kwa mara na kuboreshwa inapobidi.


Ndiyo. Kuna kiwango cha juu cha usalama kwa mionzi ya EMF kinachopendekezwa na Tume ya Kimataifa ya Ulinzi Dhidi ya Mionzi Isiyo ya Ionizi (ICNIRP).



ICNIRP hutumia kipimo cha usalama cha kuzidisha mara kumi (10) ili kupata kiwango cha juu cha mionzi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mazingira ya mionzi ya EMF na kuzidisha mara hamsini (50) kwa ajili ya kuweka kiwango kinachofaa kwa umma. 


Ndiyo. Miongozo iliyotolewa na ICNIRP kuhusu viwango vya mionzi ya EMF imeandaliwa kwa kutumia uchambuzi makini wa utafiti wa kisayansi.



Lengo ni kuhakikisha ulinzi kwa watu wote, wakiwamo watoto na wanawake wajawazito, dhidi ya athari za kiafya zinazoweza kutokea kutokana na mionzi ya EMF. Kwa mujibu wa miongozo ya ICNIRP ya mwaka 2020, wanawake wajawazito wanaofanya kazi katika mazingira yanayohusisha Masafa ya RF wanashauriwa kuepuka kuwa kwenye mazingira yanayozidi kiwango cha mionzi kilichowekwa kwa ajili ya umma, ili kuhakikisha usalama wa ujauzito wao.


Si katika mazingira yote. Vipandikizi vya kielektroniki kwa kawaida huambatana na taarifa za kiusalama kuhusu hatari au uwezekano wa vifaa hivyo kuathiriwa na mwingiliano wa vifaa vya umeme na kielektroniki ikiwa ni pamoja na simu za mkononi na vifaa vinavyotumia masafa. 



Vipo viwango maalumu vilivyowekwa kuhusu kinga dhidi ya mionzi ya masafa na mwingiliano wa masafa. Watu wenye vipandikizi vya kielektroniki wanapaswa kushauriana na wataalamu wao wa tiba kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na mwingiliano wa masafa, hasa ikiwa wanapata wasiwasi kuhusu usalama wao. Miongozo ya ICNIRP kuhusu mionzi ya EMF haina kipengele kuhusu kinga dhidi ya mwingiliano wa vifaa vya kielektroniki.


Viwango mahsusi vya ufyonzwaji wa RF “Specific absorption rate (SAR)” ni kipimo cha kiwango cha nguvu ya RF ambayo hufyonzwa  na tishu za mwili wa binadamu na hupimwa kwa kipimo cha wati  kwa kilogramu(W/Kg). Upimaji huu hutumika kubaini ikiwa simu inakidhi viwango na au miongozo ya usalama. 


Hili ni swali ambalo Shirika la Afya Duniani (WHO) wanalichukulia kwa uzito mkubwa. Ikizingatiwa idadi kubwa ya watu wanaotumia simu za mkononi, hata mabadiliko kidogo tu yenye kusababisha athari hasi kwa afya ya binadamu linaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya umma.



Ikizingatiwa kuwa mionzi ya masafa ya redio (RF) inayotolewa na simu za mkononi ni zaidi ya mara elfu moja (x1000) kuzidi ile inayotokana na minara ya mawasiliano na kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa athari kubwa zaidi kutokana na matumizi ya vifaa hivi vya mkononi, tafiti zimekuwa zikifanyika kwa umakini mkubwa kuchunguza madhara yanayoweza kutokea. Utafiti huu umelenga maeneo yafuatayo:




  • Uwezekano wa kusababisha saratani

  • Athari nyinginezo za kiafya

  • Mwingiliano wa sumaku-umeme

  • Ajali za barabarani zinazohusiana na matumizi ya simu za mkononi.



Saratani



Utafiti wa kiepidemiolojia unachunguza uhusiano kati ya mionzi ya RF itokanayo na simu za mkononi na hatari ya kupata aina fulani za saratani ya kichwa, kama vile glioma na neuroma. Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) limeainisha masafa haya ya mionzi kama yenye uwezekano wa kusababisha saratani kwa binadamu, na kuyaweka katika Kundi 2B. Ingawa tafiti zilizopo hadi sasa hazionyeshi ushahidi thabiti kwamba mionzi ya RF kutoka kwa minara ya mawasiliano inaongeza hatari ya saratani au magonjwa mengine.



Athari Nyingine za Kiafya Zinazohusiana na Matumizi ya Simu za Mkononi



Watafiti wamebaini athari za kiafya zinazotokana na matumizi ya simu za mkononi, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika shughuli za ubongo, athari kwenye stimuli za mrejesho na mifumo ya usingizi. Ingawa athari hizi zinaonekana kuwa ndogo na hazijaonyesha madhara makubwa ya kiafya, utafiti zaidi unahitajika ili kuthibitisha matokeo haya.



Muingiliano wa Umeme Sumaku



Muingiliano wa Umeme sumaku kati ya simu za mkononi na vifaa vya matibabu kama vile vifaa vya kuweka mapigo ya moyo (pacemakers), vichochezi vya moyo vinavyopandikizwa na baadhi ya visaidizi vya kusikia unaweza kuwa na athari katika utendaji kazi wa vifaa hivyo. Simu za mkononi zinapowekwa karibu mno na vifaa hivi, zinaweza kutoa mawimbi ya umeme sumaku ambayo yanasumbua mawimbi ya kawaida yanayotumika na vifaa hivi vya matibabu. Athari hizi zinaweza kupunguzwa kwa kutumia teknolojia mpya zaidi kama vile simu za 3G au zaidi, ambazo zimeundwa kutoa mawimbi yenye nguvu ndogo zaidi ya kuingiliana na vifaa vya matibabu. Kadhalika, kuna muingiliano unaoweza kutokea kati ya masafa ya simu za mkononi na mawasiliano ya kielektroniki ya ndege, jambo ambalo limepelekea baadhi ya nchi kuweka sheria na kanuni zinazodhibiti matumizi ya simu za mkononi ndani ya ndege. Hata hivyo, kuna ndege zingine ambazo zinatumia mifumo maalumu inayoweza kudhibiti athari hizi, hivyo kuruhusu matumizi ya simu za mkononi wakati wa safari bila kuathiri mifumo ya ndege.



Ajali za Barabarani



Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha chombo cha moto, iwe kwa kushikilia au kwa kutumia vifaa vya kuwasiliana bila kushikilia, husababisha ongezeko la ajali za barabarani mara tatu hadi nne zaidi ya kawaida. Ajali hizi husababishwa na ghasia zinazotokana na matumizi ya simu.



Hitimisho



Ingawa bado haijathibitishwa kama matumizi ya simu za mkononi yanaongeza hatari ya uvimbe kwenye ubongo, ongezeko la matumizi ya simu hizi na upungufu wa data za kisayansi kuhusiana na matumizi ya vifaa hivi vya mawasiliano kwa zaidi ya miaka 15 yanasisitiza umuhimu wa utafiti zaidi. Hii ni muhimu hasa kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa vijana wadogo ambao wanaweza kuwa wazi kuguswa na athari za mionzi ya ‘RF’ kwa muda mrefu zaidi, hivyo kuongeza hatari ya athari hasi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza utafiti zaidi kufanyika juu ya athari za kiafya za mionzi ya ‘RF’, hasa kwa kundi hili la watumiaji na kwa sasa linaendelea kuchambua athari hizi kwa vipimo vinavyostahili kuzingatiwa.


5G, au kizazi cha tano, ni teknolojia ya hivi karibuni ya simu za mkononi isiyotumia waya, ambayo ilianza kutumiwa kwa wingi mnamo mwaka 2019. Inatarajiwa kwamba 5G itaongeza utendaji kazi na aina mbalimbali za matumizi mapya ya teknolojia za kidijiti, ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya kwa masafa ‘telemedicine’, ufuatiliaji wa afya wa kina, upasuaji wa masafa.


5G inaleta mapinduzi katika viwango vya mawasiliano ya simu za mkononi kwa kuleta utendaji ulioboreshwa kwa kiasi kikubwa. Teknolojia hii inapanua matumizi ya masafa ya mawimbi ya redio kutoka takriban 3.5 GHz hadi masafa ya juu ya makumi ya GHz. Masafa haya ya juu ambayo ni mapya katika mitandao ya simu za mkononi, tayari yanatumika katika matumizi mengine kama vile muunganisho wa vifaa vinavyounganisha nukta moja na nyingine na skana za ukaguzi. Katika masafa haya ya juu, mitandao ya 5G inahitaji minara zaidi na vifaa vingi vilivyounganishwa ili kuhakikisha ufanisi na kasi. Zaidi ya hayo, 5G inatumia teknolojia ya antenna za beam-forming, ambazo zinaweza kuelekeza mawimbi ya masafa moja kwa moja kwenye kifaa kinachotumia mtandao, tofauti na antena za minara zinazotumika katika mitandao ya zamani kama 3G na 2G ambazo zinasambaza masafa kwa upana zaidi. Hii inaruhusu matumizi bora ya masafa na kuongeza kasi na ufanisi wa mawasiliano.



Viwango vya Mionzi



Kwa sasa, mionzi inayotolewa na miundombinu ya 5G kwenye masafa ya 3.5 GHz inalingana na ile inayotokana na minara ya simu za teknolojia za zamani, kama vile 2G, 3G na 4G. Kutokana na matumizi ya masafa mapana zaidi na antena za 5G, kiwango cha mionzi kinaweza kubadilika kulingana na eneo la watumiaji na jinsi wanavyotumia teknolojia hiyo. Ikizingatiwa kwamba teknolojia ya 5G bado iko katika hatua za awali za usambazaji, athari za mabadiliko yoyote yanaweza kutokea kutokana kuwa kwenye wigo wa Masafa ya Redio yanaendelea kuchunguzwa.


Mpaka sasa, utafiti uliofanyika umeonesha kwamba hakuna madhara ya moja kwa moja ya kiafya yanayohusishwa na mionzi ya vifaa visivyotumia waya. Matokeo ya tafiti hizo kuhusu athari za kiafya yanatokana na uchunguzi uliolenga masafa maalumu pekee. Hata hivyo, tafiti chache tu zimefanywa kuhusu athari za kiafya za masafa yanayotumika katika teknolojia ya 5G. (Ikumbukwe: muktadha huu unahusisha masafa maalumu pekee).



Kuongezeka kwa joto katika tishu za mwili wa binadamu ni athari ya moja kwa moja inayotambuliwa kutokea kutokana na mwingiliano kati ya mawimbi ya masafa na mwili wa binadamu. Viwango vya mionzi kutokana na teknolojia zilizopo sasa hivi husababisha ongezeko dogo tu la joto mwilini. Kadri masafa yanavyoongezeka, kuna upenyo mdogo zaidi ndani ya tishu za mwili na ufyonzwaji wa nishati unazidi kuhusika zaidi na uso wa mwili (ngozi na macho). Izingatiwe kwamba viwango vya mionzi wa jumla vinabaki chini ya miongozo ya kimataifa; zingatia kwamba hakuna madhara yoyote kwa afya ya umma yanayotarajiwa.


Mashirika mawili ya kimataifa yamechukua jukumu la kuandaa miongozo inayohusiana na mionzi ya sumaku-umeme. Kwa sasa, nchi nyingi zinazingatia miongozo ifuatayo:




  • Tume ya Kimataifa ya Ulinzi dhidi ya Mionzi isiyo ya Ki-ionizi (ICNIRP), na

  • Taasisi ya Wahandisi wa Umeme na Elektroniki (IEEE), ambayo hutoa miongozo kupitia Kamati yake ya Kimataifa ya Usalama wa Sumaku-umeme.



Miongozo hii imeundwa ili kuhudumia teknolojia mbalimbali na sio teknolojia maalum pekee; inashughulikia masafa yote ya mawasiliano, hadi GHz 300. Hii ni pamoja na masafa yanayotumika katika teknolojia za 5G.


WHO lilianzisha Mradi wa Kimataifa wa Sumaku-umeme (EMF) mnamo mwaka 1996. Mradi huo unachunguza athari za kiafya za mionzi



ya umeme na sumaku katika masafa ya 0-300 GHz na hutoa ushauri kwa mamlaka za kitaifa kuhusu athari za mionzi ya EMF.


Ndiyo, simu za mkononi hutoa mionzi kwa kiasi kidogo chenye vinasaba vya masafa yanayowezesha mawasiliano.


Simu za mkononi hutumia transmita za nguvu ndogo sana ambazo hutoa nishati chini ya watts 2 kwa kiwango cha juu. Simu za mkononi zimebuniwa kwa namna ambayo zinaweza kufanya kazi kwa ubora huku zikitumia nishati ya kiwango cha chini kabisa. Uwezo huu hujulikana kama ‘udhibiti wa matumizi ya nishati unaoendana na hali’.


Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!