TUNU KUU
- Weledi: Tunatekeleza majukumu yetu kwa kutoa huduma bora tukizingatia maadili na heshima kwa wateja wetu;
- Utendaji wa Pamoja: Tunaamini katika utendaji kazi wa pamoja ili kutatua matatizo na kutambua kwamba mawasiliano imara ni muhimu katika kujenga mazingira ya ushirikiano;
- Ubunifu: Tunazingatia ubunifu katika kushughulikia masuala ya kiudhibiti sanjari na mabadiliko ya teknolojia duniani;
- Uwajibikaji: Tunawajibika kikamilifu na kuchukua dhamana tunapotoa huduma;
- Uadilifu: Tunatekeleza kazi zetu kwa kuzingatia maadili, uthabiti na uaminifu wa hali ya juu.