- Kuanzisha na kuratibu utekelezaji wa sera zinazohusiana na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano;
- Kubuni Vigezo, Taratibu, Sheria, Miongozo na Kanuni za uendeshaji wa mitandao, mifumo na huduma za mawasiliano;
- Kuandaa ratiba ya kazi za Kurugenzi za kusimamia na kuratibu utekelezaji na kutathmini utendaji kazi;
- Kuanzisha na kusimamia Miundombinu Muhimu ya Umma (PKI);
- Kusimamia uendeshaji wa Tz-CERT;
- Kusimamia Utekelezaji wa masuala yanayohusiana na Usalama dhidi ya Uhalifu Mtandaoni;
- Kusimamia majukumu ya TEHAMA ya Shirika;
- Kuratibu shughuli za mashirika ya Kikanda na Kimataifa yanayohusika na maendeleo ya sekta zinazodhibitiwa kulingana na Teknolojia na Viwango