Haki za Watumiaji
- Kupata huduma nzuri
- Kupata taarifa kuhusu huduma na bidhaa
- Kutokubaguliwa
- Kutoa malalamiko
- Kusuluhishiwa malalamiko yao yote
- Uhakikisho wa usalama kwenye bidhaa na huduma wanazozinunua
- Faragha na usiri wa mtumiaji
- Kuelimishwa
- Kuarifiwa kabla ya kusimamishwa au kusitishwa kwa huduma
- Kuwakilishwa
- Kupewa taarifa sahihi kwenye ankara
- Kukata rufaa katika kesi ya kutokuridhika na huduma
Wajibu wa Watumiaji
- Kulipa ankara kwa wakati
- Kulinda mazingira kwa kuepuka kutupa vifuniko vya simu, kadi au vifaa vingine vilivyotumika ovyo
- Kugundua na kuripoti udhaifu katika utoaji wa huduma
- Kusaidia udhibiti wa habari kwa kuripoti makosa ya mawasiliano
- Kulinda vifaa na miundombinu ya mawasiliano
- Kutumia huduma zilizokubaliwa kwa haki
- Kuheshimu uhuru wa wengine kwa kutokusumbua
- Kuzingatia sheria na kanuni