JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Serikali Kupitia Upya Sheria za Mawasiliano


Serikali Kupitia Upya Sheria za Mawasiliano

 

Serikali inaandaa Sheria ya TEHAMA itakayowezesha kisheria utekelezaji wa malengo yaliyomo kwenye Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 na Tovuti Mpya ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jijini Dodoma, tarehe 01/07/2021 Waziri wa Mawasilinao na Teknolojia ya Habari Mhe.  Dkt Faustine Ndugulile Serikali inapitia Upya Sheria nyingi za Mawasiliano.

“Pamoja na kuwepo kwa Sheria mbalimbali kama TCRA, 2003, EPOCA, 2010 na e-transaction Act, 2015 na Cyber Crime Act, 2015 bado kumekuwepo na ombwe la kisheria la kudhibiti masuala ya TEHAMA kiujumla nchini. Kutokana na mapungufu yaliyopo, Serikali imeona ni vyema kutunga Sheria hii mahususi”amesema Mhe  Waziri.

Amesema lengo kuu yamabalidiko yahoo nikuendana na mabadiliko ya kiteknolojia, na kukuza ubunifu; Wizara imeandaa mkakati wa kukuza wataalamu wa TEHAMA kwenye taaluma haba mfano ‘Artificial Intelligence; Internet of Things, Big Data Analytics, uchapishaji wa 3D n.k. Aidha, chini ya Tume ya TEHAMA, Wizara itaendelea kuwatambua na kuwasajili wataalamu wa TEHAMA katika ngazi zote kama inavyoelekezwa kwenye Muundo wa Usajili wa Usajili (ICT Professional Framework).

Kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali chini ya ufadhili Benki ya Dunia, Wizara itaanzisha Kituo cha Kitaifa Kuratibu Maendeleo ya Wataalamu wa TEHAMA (National ICT Professional Development Centre) na vituo vinne vya kikanda kwa ajili ya kukuza ubunifu (Zonal Soft centers for Youth, Entrepreneurs and SMEs). Lengo la vituo hivi ni kuhamasisha ubunifu katika masuala ya TEHAMA kwa kutoa wigo mpana zaidi kwa vijana wenye vipaji katika ubunifu.

“Serikali imeendelea kuboresha muundombinu ya TEHAMA itakayowezesha kupatikana kwa intaneti yenye kasi (broadband) kwa kuongeza wigo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hadi kwenye Makao Makuu ya Wilaya.  Wizara inaongeza uwezo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mara nne kutoka 200G kwenda 800G ifikapo 2025. Ameeleza Mhe. Ndugulile.

Amefafanua kwamba, katika kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha TEHAMA, Afrika Mashariki na Kati inatarajia kuunganisha nchi ya Msumbiji ifikapo Agosti, 2021 na upembuzi yakinifu wa kufikisha Mkongo wa Taifa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia ziwa Tanganyika umeanza. Ukamilishaji wa zoezi hilo utafanya nchi zote 8 zinazopakana na Tanzania kufikishiwa Huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Lengo kuu la Serikali ni kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hadi kufikia Kilomita 15,000 na kuunganisha wilaya zote za Tanzania ifikapo mwaka 2025 na pia kufikisha asilimia 80 ya upatikanaji wa Intaneti yenye kasi ifikapo 2025.

Ameongeza kwamba, Katika kuhakikisha mawasiliano yanafika maeneo ya Vijijini na yale yaliyomo pembezoni, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), inaendelea na zoezi la uboreshaji wa Huduma za mawasiliano kutoka teknolojia ya 2G kwenda teknolojia ya 3G na zaidi ambapo itawezesha wananchi kupata intaneti yenye kasi ya kuanzia 2Mbps (Megabaiti Mbili kwa Sekunde).

Amesema, Mwaka wa Fedha 2021/22 Wizara imetengewa bajeti ya Shilingi Bilioni 211.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo. Aidha, Serikali kwa kuona haja ya kuharakisha kufikisha miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano imeongeza Shilingi Bilioni 30 kwenye bajeti ya maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa, hivyo kufikisha bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwa jumla ya Shilingi Bilioni 241.4 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Ilikutimiza azima hii, Wizara inawakaribisha wadau wote kuendelea kushirikiana na Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ule wa mradi wa Anwani za Makazi na Postikodi unaotekelezwa kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI ili kuandaa mazingira ya kuwezesha biashara mtandao. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kaya 1,975,000 na Ofisi za Umma 97,000 zinaunganishwa na Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi ifikapo Mwaka wa Fedha 2025/26 kutoka kaya 450,980 na Ofisi za Umma 48,516. Mfumo huu utawezesha urahisi wa upatakanaji wa huduma za Serikali, biashara mtandao, kuongezeka kwa mapato ya Serikali n.k

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!