JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) hutekeleza kampeni za elimu kwa umma zinazolenga kuongeza elimu ya matumizi salama na sahihi ya mawasiliano na kupunguza matukio ya uhalifu mtandaoni yanayosababishwa na ukosefu wa elimu sahihi.

1. Kampeni ya "Sambaza Mchongo na sio Uongo"

Ni kampeni ya Elimu kwa umma inayolenga kuondoa changamoto zinazowakabili watumiaji wa mawasiliano kutokana na matumizi mbalimbali ya huduma za mawasiliano ya mtandaoni. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na matumizi mabaya ya mitandao na usambazaji wa habari potofu  ambazo kwa njia moja au nyingine zinakera umma. Kampeni hii ililenga kuufikia umma wa watumiaji wa huduma za mawasiliano.  

2. Kampeni ya "Kwea Kidijitali"

Kampeni ya “Kwea Kidijiti” inalenga kukuza matumizi yenye manufaa ya huduma za mawasiliano. Kampeni hii inalenga kutatua changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma za mawasiliano, hasa zinazohusiana na matukio ya udanganyifu na uonevu wa mtandaoni. Inaongeza uelewa kuhusu Umuhimu wa kuhakiki laini za simu, kujilinda dhidi ya uonevu na udanganyifu mtandaoni, na kuhamasisha matumizi yenye tija ya huduma za mtandao.

3. Kampeni ya Uhakiki na Usajili wa Laini za Simu

Kampeni hii, ilitekelezwa nchini kuanzia Desemba 2022 hadi Machi  2023, ikielimisha watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi utaratibu wa kufuata ili kuhakiki laini zao za simu zinazotumika kwa lengo la kuimarisha matumizi salama ya huduma za mawasiliano na kuongeza utambulisho wa kipekee wa mtumiaji kidijitali. Kampeni ilishuhudia asilimia 98 ya watumiaji wakihakiki usajili wa laini zao za simu zinazotumika. TCRA inaendelea kuwahimiza watumiaji wapya wa huduma za mawasiiano kuhakikisha kwamba laini zao za simu zinasajiliwa kibayometria na kuhakikiwa. Kampeni hii iliongeza idadi ya laini za simu zilizohakikiwa na hatimaye kuchangia kupunguza vitendo vya ulaghai vinavyotokana na matumizi ya laini zisizo na utambulisho sahihi. Kampeni pia ilionyesha uhalisia wa kanzidata ya watumiaji wa huduma za Mawasiliano.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!