Makumbusho ya Mawasiliano
Makumbusho ya Mawasiliano TCRA, ilifunguliwa rasmi mwaka 2015 kwa lengo la kukusanya, kuweka kumbukumbu, kuhifadhi, kuonesha, kutafiti na kutoa elimu kuhusu historia na mabadiliko ya teknolojia za mawasiliano. Makumbusho inaonyesha historia na mabadiliko ya huduma za mawasiliano katika maeneo matano ambayo ni mawasiliano ya jadi, mawasiliano ya posta, mawasiliano ya simu, mawasiliano ya utangazaji na TEHAMA.
Makumbusho ya Mawasiliano TCRA ni kituo cha kujifunzia, kufanya utafiti na kukufanya uburudike kwa kukuonyesha vifaa mbalimbali vya kihistoria vya mawasiliano vilivyokusanywa vyenye thamani vikiakisi hatua mbalimbali za mabadiliko ya teknolojia nchini Tanzania. Vifaa vilivyokusanywa kwenye Makumbusho ya TCRA vina umuhimu mkubwa kwa wanafunzi na wanazuoni kuwawezesha kufanya utafiti kwenye sekta ya mawasiliano. Pia, makumbusho ya mawasiliano inawapokea wananchi wote.
Muda wa Kufunguliwa
Jumatatu – Ijumaa, saa 3:30 Asubuhi hadi saa 9:30 Alasiri.
Kiingilio: Hakuna
ZINGATIA: Makumbusho ipo wazi siku za kazi tu, isipokuwa siku za sikukuu za kitaifa
Vifaa vinavyoonyeshwa
- Maonyesho ya mawasiliano ya asili.
- Maonyesho ya mawasiliano ya posta.
- Maonyesho ya mawasiliano ya simu.
- Maonyesho ya utangazaji.
- Maonyesho ya vifaa vya TEHAMA
Picha na maelezo viwekwe hapa…
Ili kuchangia vifaa vya TEHAMA kwa makumbusho ya Mawasiliano, tafadhali wasiliana na Mamlaka kupitia:
Baruapepe: dg@tcra.go.tz
Simu ya bure kituo cha huduma kwa wateja: 0800008272