TCRA yakabidhi Jengo la Ofisi kwa Tume ya TEHAMA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kulia) akisaini hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Bw. Kundwe Moses Mwasaga, ambapo katika makubaliano hayo TCRA iliipatia Tume ya TEHAMA jengo la Mawasiliano lililopo eneo la Upanga, Dar es Salaam litakalowezesha utekelezaji wa shughuli za utawala za kila siku. Wanaoshuhudia ni maafisa wa TCRA na Tume.