JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Uchapishaji wa orodha ya Postikodi

UCHAPISHAJI WA ORODHA YA POSTIKODI

Kwa kuzingatia kifungu 41 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuufahamisha umma kwa ujumla kwamba orodha ya Postikodi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechapishwa kwenye Gazeti la Serikali namba 240 la tarehe 22 Aprili 2016.

Postikodi au simbo za posta ni mfumo maalum wa alama, tarakimu na herufi inayotambulisha sehemu au eneo la kufikisha huduma za posta na kwa Tanzania linaanzia kwenye kata. Upangaji wa postikodi kitaalamu umefanyika baada ya utafiti wa muda mrefu uliohusisha wataalamu mbalimbali ili kuelewa mfumo wa postikodi kwa Tanzania.

Orodha ya Msimbo wa Posta inaweza kupatikana hapa chini;

 1. Arusha 23000 (Northern Zone)
 2. Dar Es Salaam 11000 (Coastal Zone)
 3. Dodoma 41000 (Central Zone)
 4. Geita 30000 (Lake Zone)
 5. Iringa 51000 (Southern Highlands Zone)
 6. Kagera 35000 (Lake Zone)
 7. Katavi 50000 (Southern Highlands Zone)
 8. Kigoma 47000 (Central Zone)
 9. Kilimanjaro 25000 (Northern Zone)
 10. Lindi 65000 (Coastal Zone)
 11. Manyara 27000 (Northern Zone)
 12. Mara 31000 (Lake Zone)
 13. Mbeya 53000 (Southern Highlands Zone)
 14. Morogoro 67000 (Costal Zone)
 15. Mtwara 63000 (Costal Zone)
 16. Mwanza 33000 (Lake Zone)
 17. Njombe 59000 (Southern Highlands Zone)
 18. Pwani 61000 (Costal Zone)
 19. Rukwa 55000 (Southern Highlands Zone)
 20. Ruvuma 57000 (Southern Highlands Zone)
 21. Shinyanga 37000 (Lake Zone)
 22. Simiyu 39000 (Lake Zone)
 23. Singida 43000 (Central Zone)
 24. Songwe 54100 (Southern Highlands Zone)
 25. Tabora 45000 (Central Zone)
 26. Tanga 21000 (Northern Zone)
Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!