Taarifa za Utafiti
Mada za Utafiti
- Tathmini ya pamoja ya matokeo, Uchambuzi wa Mahitaji ya Huduma na Usanifu wa Mfano wa kuwezesha Mitandao Endelevu ya Vituo cha Mawasiliano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilianzisha utafiti huu kwa pamoja na Taasisi ya Maendeleo ya TEHAMA Bangladesh, yaani Bangladesh Institute of ICT in Development (BIID) na Mtandao wa Vituo vya Mawasiliano Tanzania, unaojulikana kama Tanzania Telecentre Network (TTN) ili kutathmini matokeo ya vituo vya mawasiliano na kubuni mfano wa biashara kuhudumia jamii za vijijini zilizo katka mazingia magumu kwa lengo la kuinua Maisha yao kwa kutumia nyenzo za TEHAMA. Taarifa ya uchanguzi huo inapatikana hapa (kwa kiingereza).
Uchunguzi kuhusu utoaji wa huduma za intaneti na data TanzaniaTCRA ilifanya uchunguzi kuhusu Huduma za Intaneti na Data Tanzania kati ya Aprili na Juni 2010 kwa kuhesabu watoa huduma za mawasiliano ya data katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuangalia vipengele mbalimbali. Lengo kuu la uchunguzi huu lilikuwa kuiwezesha Mamlaka na wadau wengine kuelewa maendeleo ya sekta hii na utendaji wa watoa huduma hao kwa kuangalia namna huduma za intaneti zilivyoenea na matumizi yake Tanzania. Taarifa ya uchanguzi huo inapatikana hapa (kwa kiingereza).
Uchunguzi wa Kulinganisha Gharama za Maongezi ya Simu katika nchi za Afrika MasharikiTCRA ilifanya uchunguzi wa kulinganisha gharama za matumizi ya simu katika nchi tatu: Tanzania, Kenya na Uganda. Taarifa ya uchanguzi huo inapatikana hapa (kwa kiingereza).
Uchambuzi wa Mwelekeo wa Gharama za Huduma za Simu (2000- 2006)TCRA ilifanya uchambuzi wa mwelekeo wa gharama za huduma za simu kati ya mwaka 2000 na 2006. Muhtasari wa matokeo ni kama unavyoonekana hapa chini ( kwa kiingereza):