Mwanzo
Kuhusu
Huduma
Viunganishi
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Habari

Makabidhiano ya Ofisi Kati ya Menejimenti Iliyomaliza Muhula Wake Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Arusha, Tanzania


Makabidhiano ya Ofisi Kati ya Menejimenti Iliyomaliza Muhula...

 

  • MEJIMENTI MPYA YAANZA KAZI MAKAO MAKUU YA PAPU

Menejimenti mpya ya chombo cha sekta ya posta barani Afrika, Umoja wa Posta Afrika (PAPU) imeanza kazi leo, tarehe 1 Septemba 2021 kufuatia sherehe iliyofana iliyofanyika kwenye jengo la uwekezai PAPU, makao makuu Arusha mjini mkoani Arusha.

Katibu Mkuu WA PAPU aliyemaliza muhula wake, Bwana Younouss Djibrine; alikabidhi uongozi kwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja huo, Bwana Sifundo Chief Moyo kwenye shughuli ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Dr. Faustin Ndugulile (Mb.).

Kma sehemu ya mabadiliko ya uongozi katika chombo hicho cha bara la Afrika, Katibu Mkuu Msaidizi aliyemaliza  muhula wake kwenye Umoja huo, Bwana Kolawole Aduloju  pia alikabidhi ofisi kwa Bi. Jessica Hope Uwera Sengooba.

PAPU inaendele kutekeleza majumumu yake muhimu  ya kujenga ENEO MOJA LA SHUGHULI ZA  POSTA wakati wote na katika mazingira yote, kama mchango wake kwenye kufikia azma ya pamoja na ya muda mrefu ya watu wa Afrika ya kuleta maendeleo shirikishi na endelevu kwa jamii.

Mabadiliko ya menejimenti ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) yameainishwa kwenye utaratibu rasmi wa kukabidhiana madaraka kwa mpangilio baada ya kumalizika kwa muhula wa uongozi wenye mafanikio makubwa.

Menejimenti mpya inaingia ofisini kipindi cha janga la UVIKO-19 ambalo limevuruga shughuli za mifumo ya shughuli za kibiashara na ambalo linahofiwa kuleta athari za muda mrefu kwenye maendeleo ya kawaida ya biashara na kwa hivyo kuibua changamoto kwa umma kwa ujumla kutathmini upya njia bora za kukabili athari hizo.

Mikakati ya kutathmini upya na kukabili hali hii inahitajika ili kuweza kugeuza changamoto zilizojitoketa kuwa fursa kwa ama kubadilimifumo ya utoaji huduma au kubadili bidhaa na huduma zinazotolewa ili kuendelea kuwa na wateja na hivyo kuendeleza biashara. Hii itachangia katika kulinda sekta ya posta na kuimarisha uwezo wake wa kugundua mapema na kukabiliana na majanga mengine kama haya mbeleni.