JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni Mlezi wa Sekta ya Mawasiliano-Nape

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni Mlezi wa Sekta ya Mawasil...

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye amesisitiza kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itasalia kuilea sekta ya Mawasiliano nchini, ili kuhakikisha inatoa mchango chanya katika Ujenzi wa uchumi wa Kidijitali.

Akizungumza katika mahoajiano yaliyofanyika katika kituo cha televisheni cha E jijini Dar es salaam mapema wiki hii Waziri Nape alisisitiza kuwa kazi ya Mamlaka hiyo ni kufanya uchambuzi wa taarifa za kimtandao na suala la uhalifu unaotendeka mtandaoni si suala lake bali linasimamiwa na kutekelezwa na Jeshi la Polisi Tanzania.

“TCRA hawakamati kabisa,siyo kazi yao kukamata; marufuku TCRA kukamata; hata kama unatokea uhalifu mtandaoni, kazi yao siyo ya kukamata, ni kufanya uchambuzi kusema huyu Fulani ni nani, anafanya nini na nini, halafu kazi ya kukamata ni kazi ya vyombo vingine kama Polisi nakadhalika,kwa hiyo sisi TCRA ni facilitator (mwezeshaji), tunaku facilitate (tunakuwezesha) wewe umjue mtu” alisisitiza Nape.

Waziri Nape alisisitiza kila mtumiaji wa huduma za Mtandao kuhakikisha anazingatia matumizi sahihi na salama ya mitandao kwa kuwa maudhui kwenye Mtandao yanaishi dahari.

“Hakuna jambo mtandaoni haliachi alama, usijisahau; watu wengi naona wanakosa kazi, wanakosa nyaraka Viza (nyaraka za kumwezesha mtu kusafiri na kuishi ugenini), kwa sababu watu wakienda ku-trace (kuchunguza) mtandaoni, wakitazama kurasa zake za mitandao ya kijamii wanajikuta wanakosa sifa,” aliongeza Waziri Nape na kutahadharisha.

Alisisitiza kuwa Mamlaka hiyo itaendelea kuweka kipaumbele utoaji wa elimu kwa wenye leseni za Mawasiliano, badala ya kuweka kipaumbele utoaji wa adhabu kwa watoa huduma za Mawasiliano wanaobainika kukiuka masharti ya leseni na miongozo mingine inayowaongoza.

“TCRA imebadilika sana; adhabu zimepunguzwa, na nimewasisitiza kwa ‘jamani nyie ni walezi’ watoa huduma wakikosea waiteni, zungumzeni nao, kipaumbele kisiwe adhabu kabla ya maelekezo na mazungumzo,” alibainisha Nape.

Kauli ya Waziri imekuja ikiwa ni utaratibu uliowekwa kimataifa kuhakikisha, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinanatoa elimu na hamasa kwa watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutumia huduma hizo kwa tija na kuepuka matumizi ya huduma hizo yasiyokuwa salama.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!