JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Jengo jipya Umoja wa Posta Afrika mfano mabadiliko kidijitali


Jengo jipya Umoja wa Posta Afrika mfano mabadiliko kidijital...

 

Mfano wa mchango kwenye juhudi za sekta ya Posta Afrika kuelekea mabadiliko kidijitali kwenye utoaji huduma unaonekana Arusha, kupitia jengo la kisasa litakalokuwa makao makuu ya taasisi mahsusi kwa kushughulikia masuala ya posta katika Bara hili.

Umoja wa Posta Afrika (PAPU), ambao unatekeleza mikakati ya kuendeleza biashara mtandaao Barani humu, sasa umepata jengo la makao makuu lililojengwa kwa mabilioni ya shilingi na ambalo ni kivutio kwa usanifu na mwonekano wake, ulio kama stempu.

Jengo hilo jipya, lenye nafasi ya ofisi na maeneo ya biashara, na ambalo linaendeshwa kwa teknolojia za kisasa, litazinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 2 Septemba mwaka huu. 

Kwa Arusha, jiji linalojulikana kwa sifa ya kuwa kituo cha mikutano ya kimataifa kama vile ilivyo Geneva, jengo hilo ni johari nyingine kwenye taji lake. Tanzania iijitolea kuwa mwenyeji wa PAPU Umoja huo ulipoanzishwa tarehe 18 Januari 1980 mjini Arusha.

Jengo hili jipya la PAPU limejengwa kwa ubia kati ya Umoja huo na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Umilki ni asilimia 60 PAPU na 40 TCRA.

TCRA, msimamizi wa sekta ndogo ya posta nchini, ni mdau mkuu katika mradi huu na inawakilisha Serikali kwenye masuala ya kuhudumia PAPU.

Kukamilika kwa jengo hili kumewezekana miaka mitatu baada ya kuwekwa jiwe lake la msingi, sherehe iliyofanyika tarehe 18 Janauari 2020, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya PAPU. Aliyekuwa Waziri wa Tanzania wa Ujenzi, Usafirihaji na  Mawasiliano, Mhandisi  Isack Kamwelwe, aliweka jiwe hilo kwa niaba ya Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania.

Jengo hili limebadilisha mandhari ya jiji la Arusha. Mfano wa stempu ya kidijitali unaonekana kwa wanaoingia jiji hili kutoka sehemu tofauti na ukiwa juu yake unapumia hewa safi na kuona jiji la Arusha kwa chini, ikiwa ni pamoja na ardhi na mashamba,miti na bustani na vijito vinavyotiririka maji kutoka Mlima Meru, ambao ni wa pili kwa urefu Tanzania baada ya Kilimanjaro ulio jirani.

Majengo ya PAPU yako katika mita za mraba 22,421; kando ya barabara kuu kutoka Moshi kuelekea Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya. Arusha ni lango kuu cha kuingilia maeneo ya vivutio vya kitalii, vikiwa ni pamoja na mbuga ya wanyamapoti ya Serengeti na eneo la uhifadhi  la Ngorogoro, ambalo litambuliwa kimataifa kama Urithi wa Dunia.

Huduma nyingi kwenye jengo hilo  la PAPU zinaendeshwa kwa kutumia tenolojia ya kisasa, ambazo zinawezesha mtumiaji kupata huduma kwa ufanisi wa hali ya juu.

Jengo kuu lenye ghorofa 17 lina sehemu ya chini ya ardhi, ofisi za kisasa, eneo la shuhuli za biashara  na maegesho yenye uweo wa magari 137, yaani 37 hilo enelo la chini ya ardhi na 130 kuzunguka jengo. Kuna seti tatu za majenereta ya umeme kwa ajili ya dharura. Pia kuna matenki ya kufadhia maji -ya juu ya paa yenye uwezo wa ujazo wa lita 7,200 na chini ya ardhi yenye uwezo wa lita 210,000.

Vilevile kuna ukumbi wa mikutano wenye vifaa vya kisasa vya kidijitali, unaoweza kuingia washiriki 400 kwa mara moja. Pia kuna vyumba vitano vya mikutano midogo vyenye uwezo wa washiriki 30 kila kimoja.

Uamuzi wa kuwa na jengo la kisasa la PAPU ulifanyka kwenye mkutano wa 29 wa kawaida wa mawaziri wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru Afrika (OAU), ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU) Julai 1977 jijini Libreville, Gabon. Walipitisha azimio namba CM/Res. 586(XXIX) ambalo lilipendekeza kuansishwa kwa PAPU kuwa chombo cha juu cha kusimamia masuala ya Posta Afrika.

Azimio hilo liliidhinishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa OAU kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Libreville Julai 1977.  

Tarehe 7 Oktoba 1984, PAPU na Serikali ya Muungano wa Tanzania ziliingia mkataba ulioainisha masharti na vipengele vingine vya kuweka makao makuu ya Moja huo Arusha. Hili lilifuatia kutolewa idhini na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tarehe 24 Septemba 1984; hivyo kufungua njia ya PAPU kuwa na makao yake makuu Arusha.

Kwa kipindi kirefu, huduma za Posta Afrika zimekuwa na majukumu ya kipekee, kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya nchi za bara hili kujipatia uhuru.

 Katika ujumbe wake siku ya Posta Afrika tarehe 18 Januari 2023, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri K. Bakari alieleza kwamba ushirikiano baina ya nchi kupitia huduma za Posta umekuwa na umuhimu mkubwa katika kujenga mazingira ya biashara. Ili kufanikisha na kuwezesha hili, Tanzania hivi karibuni imekaribisha uwezeshaji wa huduma za posta kati yake na nchi nyingine kupitia mipaka.

PAPU inasisitiza utayari wake wa kubadili huduma za Posta Afrika kuwa kichocheo cha biashara mtandao kati na baina ya nchi.

Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bwana Sifundo Chief Moyo alisema kwenye ujumbe wake Siku ya Posta Afrika mwaka huu kwamba hili litawezekana kupitia mabadiliko ya kidijitali katika uendeshaji shughuli za posta na kuzifanya kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia ili kufungamanisha utoaji wa huduma. 

Posta imechukua mwelekeo tofauti  kufuatia kushuka kwa idadi ya barua na kuongezeka kwa vifurushi vinavyosafirishwa kama sehemu ya biashara mtandao. Sekta ya Posta inabidi kuelekeza juhudi zake, kupanga upya uwezo  na mwelekeo wake na pia raslimali zake, ili kujiweka tayari kutoa huduma kama chombo kinachotegemewa kusafirisha vitu na kufikisha huduma, alifafanua.

Posta zinatakiwa kuchukua fursa ya kukua kwa biashara mtandao na masoko yanayojitokeza kuongeza vyanzo vya mapato yao na kujijengea uhalali miongoni mwa jamii zinapotoa huduma. Vituo vya posta zaidi ya  37,000 vilivyoenea Barani Afrika ni sehemu za kuanzia kupanua huduma kuoitia mifumo ya kidijitali kuelekea kuwa na posta zenye hadi za  kisasa, alisema Katibu Mkuu huyo.

“Kwa kupata na kutumia programu za kidijitali kuendesha posta na kutoa huduma kupitia intaneti na vifaa vya mkononi kama vile simu janja, vishkwambi, komputa mpakato, Posta zinaweza kuongeza uwezo wa kutoa huduma kwa uganisi zaidi.” aliongeza.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!