TAARIFA KWA UMMA: WITO KWA WASICHANA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UMAHIRI KATIKA TEHAMA, MWAKA 2022.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuwatangazia na kuwakaribisha wasichana wenye Taaluma ya TEHAMA waliotengeneza au kubuni mradi wa TEHAMA unaotatua changamoto katika jamii, kushiriki Shindano la Umahiri wa TEHAMA kwa Wasichana litakaloambatana na maadhimisho ya Siku ya TEHAMA kwa wasichana (Girls in ICT Day), tarehe 28 Aprili, 2022.
Ili kushiriki tafadhali jaza fomu kupitia https://edodoso.gov.go.tz/index.php/915293?lang=en.
Mwisho wa kujisajili ni tarehe 13 Machi, 2022.