JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Tanzania Kujenga Chuo Bora Chakisasa Cha Tehama


Tanzania Kujenga Chuo Bora Chakisasa Cha Tehama

SERIKALI inatarajia kujenga Chuo Bora Zaidi chakisasa cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hapa Nchini ili kuongeza Kasi, Ubunifu na Ufanisi katika matumizi ya TEHAMA.

Akizungumuza katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021, Kwenye Viwanja vya Magufuli, Wilayani Chato, Mkoani Geita, tarehe 14-10-2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, alisema kwamba Dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda ambapo shughuli nyingi duniani za kiuchumi na kijamii zinafanyika kwakutegemea TEHAMA.

Mheshimiwa Rais alielezea kufurahishwa kwake na Kaulimbiu ya Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, 2021 ambayo inahimiza matumizi sahihi ya TEHAMA:-“TEHAMA ni Msingi wa Taifa endelevu; itumike kwa Usahihi na Uwajibikaji.” Kauli mbiu hii imejikita katika kuhimiza matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Rais Samia amesema TEHAMA imewezesha shughuli nyingi kurahisishwa katika upatikanaji wake. Huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kama vile Ufugaji, Kilimo, Uvuvi, Afya, huduma za kibenki, uchimbaji madini,  ulipaji wa bili za maji na nishati ya umeme kwa njia ya mtandao, ulipaji wa kodi na mapato ya Serikali, urahisashaji wa upatikanaji wa huduma za afya na tiba, elimu, huduma za Vipimo, masoko, biashara, taarifa za hali ya hewa na upatikanaji wa taarifa mbalimbali na kupunguza upotevu wa mdana na gharama za kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya kupata huduma na mahitaji mbalimbali.

Alisema katika kudhihirisha umuhimu katika matumizi ya TEHAMA, hivi majuzi kulitoea itirafu katika matumizi ya mitandao ya kijamii kama, Facebook, Instagramme na WhatsApp, ambapo dunia nzima ilisimama. Aliongeza kwamba kwa mda mfupi, mmiliki wa mitandao alitangaza kupata hasara ya Dola za Kimerikani Bilioni Saba, sawa na Shilingi Trilioni 15 za Kitanzania, kutokana na mitandao hiyo kutokuwa hewani kwa mda wa Saa sabatu. Hapa nchini pia wamiliki wa biashara wengi walipata hasara baada ya shughuli zao kuvurugika kwakukosekana mawasiliano ya mtandao.

Nikwakutambua umuhimu na nguvu ya TEHAMA kwenye dunia ya sasa, Tanzania nayo imeamua isibaki nyuma, kwa kiuwekeza kiasi kikubwa cha fedha, katika huduma mbalimbali kwenye sekta hiyo ikiwemo ujenzi wa Miundombinu ya Mkongo wa Taifa na kuusogeza hadi Kila Wilaya.  Pia Serikali imeondoa VAT kwenye vifaa vya TEHAMA na Kieletroniki kama simu janja, vishikwambi na modemu ilikuwajengea vijana mazingira bora ya kutumia TEHAMA kujiajiri kwa maendeleo yao.

“Zaidi ya hapo, Serikali inajipanga kujenga Chuo Kikubwa sana cha TEHAMA tumejipanga kutoa kipau mbele kwenye masuala ya Utafiti na Ubunifu kwenye TEHAMA, tutawasajili na kuwatambuwa vijana wote wanaojishughulisha na TEHAMA.” Rais Samia aliahidi kwamba Serikali yake, itatoa kipaumbele katika kusaidia vijana wataojiunga pamoja kwenye shughuli mbalimbali za utafiti na ubunifu kwenye TEHAMA, kwa ajili ya kujengea uwezo wa Kimataifa, kujiingizia kitapato na kwa maendeleo ya Taifa. “ Nahivyo tutakwenda kujenga chuo kikubwa sana cha TEHAMA, Chuo ambacho nadhani kwa Africa Mashariki na Kusini kwa Afrika Tanzania itakuwa inaongoza.”  Alisema Mhe. Rais.

Alisema kwamba, “ richa ya manufaa mengi ya TEHAMA, niwazi kuwa ikitumika vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo mifarakano, vurugu, machafuko, vita, na pia kuongezeka vitendo viovu, kamavile wizi wa kimtandao,  ugaidi, utakatishaji fedha nakadharika, kwa hiyo vijana ndio waadhirika wakubwa wa matumizi mabaya ya TEHAMA. Vitendo hivi vinavuruga amani, utulivu na mshikamano wa Nchi yetu.  Kwahiyo basi, niungane na kauli ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuwataka vijana wajiepushe na matumizi mabaya ya Mtandao.

Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, 2021 Wilayani Chato, kilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 22, ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa ambapo hutumika kuwawezesha vijana kutafakari falsafa, maono pamoja na kazi za Baba wa Taifa alizozifanya kwa uzalendo mkubwa kwa nchi yetu.

Vijana ni kundi lenye uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu, kundi lenye ubunifu, uthubutu, ujuzi na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja. Kwa misingi hiyo, vijana ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa.

Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, pia inalenga kwakumbusha Vijana na kuiwezesha jamii na Taifa kwa ujumla kutambua mchango mkubwa wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye alitoa mchango mkubwa katika kulikomboa Taifa letu akiwa kijana.  Kwahiyo, vijana wote nchini ni lazima watambue kuwa Taifa letu linawategemea sana katika kudumisha amani,uzalendo, umoja, mshikamano wa Kitaifa, uchapaji kazi na usimamizi thabiti wa rasilimali za Taifa kwa maendeleo Wananchi na Taifa.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!