JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Tanzania yapata kiti katika Baraza la ATU huku ikilenga kupata uungwaji mkono katika uchaguzi kwenye Baraza la ITU


Tanzania yapata kiti katika Baraza la ATU huku ikilenga kupa...

 

TANZANIA imepata uanachama wa Baraza la Umoja wa Mawasiliano Afrika (ATU) kwa kipindi cha miaka minne ijayo baada ya wajumbe wa mkutano mkuu kuipitisha kwa kauli moja; Shukrani kwa juhudi za Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mheshimiwa Nape Nnauye (Mb).  Mheshimiwa Nape aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa sita wa Umoja huo uliofanyika Algiers, Algeria Julai 2022 .

"Kati ya wanachama 49 wa Umoja wa Mawasiliano wa Afrika (ATU), Tanzania ilikuwa mojawapo ya mataifa 25 pekee yaliyopata hadhi hiyo," taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mwezi Julai ilifafanua.

Tanzania itaketi kwenye kiti hicho katika kipindi kinachoanzia mwaka 2023 hadi 2026.

Katika hatua nyingine, raia wa Kenya John Omo aliidhinishwa kuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa ATU kwa muhula mwingine ujao wa miaka minne baada ya kuhitimisha kipindi chake cha awali chauongozi wa taasisi hiyo. OMO alishinda wadhifa huo baada ya kutangulia mbele kwa kura dhidi ya mshindani wake rai awa Mauritania, Bw. Mohamed Ahmed Ould Abderrahmane.

Mkutano Mkuu huo, ambao huketi kila baada ya miaka minne katika kikao cha kawaida, ni chombo kikuu cha ATU kinachoundwa na wawakilishi walioidhinishwa rasmi wakiwemo Mawaziri wa kisekta wa Nchi Wanachama wanaohusika na mawasiliano. Ili kufikia malengo ya ATU, mkutano mkuu unaweka pamoja na mambo mengine sera mbalimbali ambazo Muungano au wanachama wake wanapaswa kuzipitisha na kuzitekeleza.

Kwa kuwa mjumbe wa Baraza, inatazamiwa kuwa taifa hilo la Afrika Mashariki litakuwa katika nafasi kubwa zaidi ya kupata nafasi kubwa ya uungwaji mkono katika Halmashauri Kuu ya ITU al’maarufu ITU PP-22 itakayokutana kwenye mkutano wao wa Septemba nchini Romania katika jiji la Bucharest.

Tanzania ni mwanachama wa Kundi ‘D’ la ITU na itatafuta kuungwa mkono na wanachama wenzake wengine katika mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya ITU.

Kundi ‘D’ katika ITU linajumuisha mataifa ya Afrika zikiwemo nchi za Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, Misri, Ghana, Kenya, Mauritius, Morocco, Niger, Nigeria, Rwanda, Senegali, Afrika Kusini, Tanzania, Tunisia, na Uganda, ambapo Tanzania, Misri, Ghana, Kenya, Nigeria, Rwanda, na Uganda zinawania kuingia kwenye Baraza hilo la ITU.

Tanzania imeahidi kuwa: Itasimama kikamilifu kuhakikisha ITU inafikia malengo yake kwa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama, mashirika ya kikanda na kimataifa; Kuhakikisha maendeleo ya viwango vya kiufundi na ugawaji wa rasilimali adimu za mawasiliano kulingana na mwongozo wa vyombo vya ushauri vya ITU na maazimio ya nchi wanachama; kuunga mkono juhudi za pamoja kati ya nchi wanachama ili kukuza muunganisho wa kidijitali kwa kuhakikisha ufikivu, upatikanaji na uwezo wa kumudu huduma za mawasiliano; na Kuhakikisha maendeleo ya viwango vya kiufundi na ugawaji wa rasilimali adimu za mawasiliano kulingana na mwongozo wa vyombo vya ushauri vya ITU na maazimio ya nchi wanachama.

TCRA inatambulika kwa mchango wake mkubwa katika kukuza maendeleo ya mawasiliano katika ukanda wa Afrika, hasa kusini mwa Sahara. Pia inawakilisha Tanzania katika taasisi mbalimbali za mawasiliano duniani kote na ni mwanzilishi mwenza wa taasisi kadhaa za mawasiliano za kikanda na Afrika.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!