JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

TCRA ya Himiza Umakini katika Matumizi ya Mtandao


TCRA ya Himiza Umakini katika Matumizi ya Mtandao

Na mwandishi wetu

KATIKA zama za Taarifa na Uchumi wa Kidijiti ambapo kila kitu kutoka masuala ya kibanki hadi burudani hufanyika mtandaoni, Usalama wa Mtandao nimuhimu zaidi kuliko hapo awali.

Kadri Taifa linavyoenda sambamba na mabadiriko ya kidijitali, kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wanao unganishwa mtandaoni. Huduma salama za mtandaoni nisuala la msingi hasa katika kutengeneza  mtandao uliosalama kwa wote.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejenga mifumo wezeshi ambapo Wananchi wameendelea kunufaika na huduma mbalimbali ninazotolewa kwa Ubora, Kazi kubwa na Ufanisi kupitia mfumo wa mtandao zikiwemo na huduma za kutuma na kupokea hela kwa kupitia simu za mkononi, kunuwa umeme, kulipitia matibabu, maji na kuuza bidhaa za aina mbali mbali.

TCRA imewakumbusha Watanzania kuwa macho na kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni, ikiwa ni pamoja na kutojibu taarifa wanazotumiwa bila ridhaa zao kabla ya kuhakiki vyanzo vyake.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari amesema Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwamba mazingiza salama mtandaoni yatawezesha Watanzania kufikia malengo yao ya kiuchumi na ya uraia.

TCRA imezindua kampani kabambe ijulikanayo “Ni Rahisi Sana” inayolenga kuelimisha Wananchi namna ya kubaini na kutambuwa matapeli na wezi mtandaoni. Kampeni hii inalenga maeneo mengi ambapo itaiendesha kote nchini kuinua kiwango cha uelewa wa umma kuhusu fursa za mtandao wa intaneti na usalama wake.  Kampeni hiyo ya awamu mbili itatekelezwa kati ya Oktoba na Desemba 2024, na Januari na Machi 2025 mtawalia.

Mamlaka hiyo itatoa mbinu na maarifa ya usalama mtandaoni. Dkt Bakari amesema Mamlaka pia itawataka watu binafsi na taasisi zaidi kutumia kikoa cha Tanzania kwenye tovuti zao na anwani za barua pepe. 

Kampeni pia inahusisha namna ya kugundua maudhui mitandaoni yanayolenga kupotosha, na pia jinsi ya kugundua habari feki. Walengwa watafundishwa pia njia za kutoa taarifa za uhalifu mtandaoni.

Vilevile kampeni inaendeleza uelewa wa wadau kuhusu klabu za kidijiti na ubunifu. TCRA imeanzisha na inaratibu uanzishaji wa klabu za kidijiti ili kuendeleza uelewa wa masuala ya kidijiti kuanzia ngazi ya elimu ya chekechea hadi vyuo vikuu.

Ubunifu na ulinzi wa wadau ni mojawapo ya masuala muhimu yanayosisitizwa kwenye Mpango mkakati wa TCRA unaotelekezwa kati ya mwaka wa fedha 2021/2022 na 2025/2026.

Dkt. Bakari amesema TCRA imeandaaa ujumbe mahsusi kwa kila eneo la kuongeza elimu. Ujumbe utatolewa kupitia vyombo vya habari, meseji fupi kwenye simu za mkononi, na kwenye maeneo ya umma ikiwa ni pamoja na mabasi, treni na vivuko. Vilevile utatolewa  kwenye maonesho na semina.

Amefafanua kwamba ingawaje mipango ya kuongeza uelewa wa umma ni ajenda ya kudumu ya TCRA, kampani hii inatokana na umuhimu wa kipekee kuwapatia Watanzania mbinu za kujilinda dhidi  ya mashambulio ya mitandao ya intaneti na simu.

Amesema TCRA inajitahidi kuelimisha umma kuhusu usalama na uimara wa mitandao na matumizi bora, ambapo wananchi wanahimizwa kutuma kwa ujumbe mfupi, wapatapo namba ya tapeli kwenda namba “15040” huduma hii ni BURE.

Kuendeleza elimu ya masuala ya kidijiti na usalama mtandaoni kunahakikisha kuwepo mazigira salama na imara ya matumizi ya mitandao, aliongeza.

Kampeni hii inafuatia mpango mwingine wa TCRA kuhamasisha watu na taasisi kutumia kikoa cha Tanzania, yaani dot tz kwenye tovuti zao na anwani za barua pepe.

Mpango huo ulieleza faida za kikoa cha Tanzania, ikiwa ni pamoja na tovuti husika kupatikana kwa urahisi wahusika wanapotafuta vitu au kuduma zinazotolewa na Watu au kampuni za Tanzania.

Matumizi ya  kikoa cha Tanzania pia yanaonesha weledi wa mwenye tovuti na pia inatoa fursa za kujitangaza na kujijenga kibiashara. Vilevile yanajenga imani ya watumiaji wa huduma husika, hivyo kuwezesha mwenye kikoa kupanua wigo wa  wateja.

Kampeni hii ya sasa imezinduliwa mwezi mmoja baada ya ripoti ya Shirika la Mawasiliano Ulimwenguni (ITU) kuitaja Tanzania kama mojawapo ya vinara 46 wa usalama mitandaoni kwa mwaka 2023.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya ITU, inayoitwa Fahirisi ya Dunia ya Usalama mtandaoni, Tanzania inaongoza nchi za Mashariki na Kati mwa Afrika kwa viwango vya juu vya usalama mitandaoni.

Tanzania imepanda viwango kutokana na ufanisi katika kusimamia misingi mitano ya usalama mitandaoni. Hii ni pamoja na utoaji wa elimu na kuongeza uwezo wa watu katika masuala ya usalama mitandaoni.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!