JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

TCRA yaendelea kuwa Kisima cha Maarifa kwa Mamlaka nyingine Afrika


TCRA yaendelea kuwa Kisima cha Maarifa kwa Mamlaka nyingine...

 

Ujumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano ya Mali (AMRTP) umefika katika Ofisi ya makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika Sekta ya Mawasiliano.

Ziara hiyo ya mafunzo ya siku mbili iliyoanza Jumanne tarehe 03 Oktoba 2023 hadi jumatano tarehe 04 Oktoba 2023 iliangazia maeneo mbalimbali ikiwemo Huduma za Fedha Mtandao, Uthibitishaji wa Vifaa vya Mawasiliano na Usimamizi wa Rasilimali Kikoa cha Hadhi ya Juu.

Walipowasili makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam, ujumbe huo kutoka Mali ulikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilano Tanzania (TCRA) Dkt Jabiri K Bakari ambapo aliwakaribisha na kuwatakia mafunzo mema na kuwasihi watembelee vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama na Visiwa vya marashi ya karafuu na Uchumi wa Buluu, Zanzibar.

Kwa upande wao ujumbe huo ulioongozwa na Cisse Ahmadou Dit Adi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Simu na Intaneti wamesemeishukuru TCRA kwa ushirikiano na mafunzo waliyopata ambayo wamesema yataenda kuimarisha zaidi utendaji wao na sekta ya mawasiliano na wanatazamia kujipanga zaidi kuimarisha ushirikiano na TCRA ili kuwa na ziara nyingi zaidi za mafunzo na kubadilishana uzoefu. "Temejifunza mengi TCRA na tunaahidi kurudi tena kwani Tanzania imefanikiwa sana katika maeno ya huduma za fedha mtandaoni” alibainisha.

Huu ni mwendelezo wa Mamlaka ya Mawasiliano kupokea wageni kutoka Mataifa mbalimbali ambao wanakuja nchini kujifunza masuala mbalimbali ya sekta ya mawasiliano ambapo mwezi September 2023 TCRA ilipokea ujumbe mwingine kutoka Mamalaka ya Mawasiliano nchini Msumbiji (INCM) uliokuja Tanzania kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo utoaji wa leseni.

Nchi nyingine zilizonufaika na mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa kuleta wataalamu nchini Tanzanaia ni  Malawi, Msumbiji, Zambia, Botswana, Rwanda na Burundi.

 

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!