JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Tunafanyia kazi Maoni ya Wadau wa Sekta Ndogo ya Utangazaji kuhusu Uboreshaji wa Sekta hiyo - Serikali


Tunafanyia kazi Maoni ya Wadau wa Sekta Ndogo ya Utangazaji...

 

Serikali imeahidi kufanyia kazi maoni ya uboreshaji wa huduma za Utangazaji   yaliyotolewa na wadau katika kikao cha mashauriano ya jinsi ya kuboresha huduma za Utangazaji nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, ambacho kiliunganisha wadau kutoka maeneo mbalimbali  ya Tanzania,  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jimmy Yonazi amesema Serikali  iko tayari kujifunza kutoka kwa wadau hivyo washiriki wawe huru katika kuchangia.

Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kimekusanya maoni katika maeneo matano ambayo ni pamoja na tozo za leseni za Redio, Televisheni, Maudhui mtandaoni na Masafa ya Utangazaji.

Maeneo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na mfumo wa biashara kwenye urushaji wa matangazo ya televisheni yanayorushwa bila kulipia na mfumo wa biashara kwenye matangazo ya televisheni ya kulipia.

Aidha, matumizi ya kisimbusi kimoja ili kupata maudhui kutoka kwa watoa huduma tofauti; mikataba ya kibiashara kati ya vituo vya utangazaji na wasambazaji wa matangazo; na wajibu wa vituo hivyo katika leseni pia vimejadilidiwa.

Hii ni mara ya sita kwa mwaka huu 2021 ambapo TCRA imekuwa ikiandaa mikutano ili kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kuboresha huduma za Mawasiliano.

Je, una Maswali yoyote juu ya Sekta ya Mawasiliano?
Tuma Mrejesho na Malalamiko!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wake wote.

Tuma Mrejesho na Malalamiko!