Hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa na mtumiaji katika kusajili laini ya simu kwa njia ya biometria.
Unaweza kuthibitisha kuwa umesajiliwa kikamilifu kwa kupiga *106#.
Lengo la usajili kwa kutumia mfumo wa biometria ni kuimarisha usalama katika matumizi ya simu za mkononi, kulinda watumiaji na kufanikisha shughuli zingine za usimamizi wa sekta ya mawasiliano.
Mteja anatakiwa kufuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko. Kwanza, wasilisha malalamiko yako kwa mtoa huduma wako, endapo malalamiko hayatashughulikiwa au kusuluhishwa wasilisha malalamiko hayo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Fedha za mtu aliyefariki zilizopo kwenye akaunti au simu yake hupatikana kwa kufuata utaratibu wa mirathi kama ilivyo kwenye mali nyingine. Hivyo basi mtu aliyeteuliwa kusimamia mirathi anajukumu la kuchunguza na kukusanya mali zote za marehemu ikiwa ni pamoja na fedha za zilizopo kwenye simu yake ya mkononi au kwenye akaunti za benki.
Malalamiko yanye sura ya Jinai Kisheria yanashugulikiwa na Jeshi la Polisi Tanzania. TCRA inashauri ufungue Kesi Polisi ili suala lako liweze kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Malalamiko yanye sura ya Jinai Kisheria yanashugulikiwa na Jeshi la Polisi Tanzania. TCRA inashauri ufungue Kesi Polisi ili suala lako liweze kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inakufahamisha kuwa michezo yote ya bahatisha husimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania GBT). Hivyo inakushauri uwasiliane na GBT kwa kutumia namba 0800110051 (bila malipo) kwa msaada zaidi na utatuzi wa lalamiko lako.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inakushauriwa kupata ripoti ya upotevu (lose report) kutoka Jeshi la Polisi yenye taarifa kamili ya kifaa chako ikiwa ni pamoja na namba tambulishi (IMEI) yake na uthibitisho wowote mwingine kuonyesha umiliki wa simu husika, kisha nenda kwa Mtoa Huduma wako wa SIM card liyokuwa ndani ya simu kabla ya kuibwa na kisha uombe kufunga simu husika.
Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inakufahamisha kuwa masuala yote ya kijinai yanashughulikiwa na Jeshi la Polisi. Unashauriwa kuripoti kituo cha polisi kupata RB na Mpelelezi kwa ajili ya hatua stahiki. Kukiwa na kikwazo chochote ongea na Mkuu wa kituo au ngazi zinazofuata mpaka upate suluhisho.
Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.
Tanzania Communications Regulatory (TCRA) would like to inform that all issues related to fraud including fraud that is conducted through telecommunication is resolved by Police. TCRA advises a person who has encountered fraud to report the incident to Police station in order for Police to register the incident by providing an RB number and additionally, Police to assign an investigator who will be responsible for investigating the matter.
Additionally TCRA would like to inform all who encounter fraud when using telecommunication services are advised to report the telephone numbers involved in fraud by writing SMS with keyword “UTAPELI” to number 15040. After sending the keyword to 15040 a notification will appear requesting to enter the phone numbers that were involved in fraud and here a subscriber should enter the phone number that were involved in the fraud incident that he/she encountered.
For more information or clarification consumers can contact TCRA by toll free number 0800008272 or by email- dawatilahuduma@tcra.go.tz
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, inakufahamishwa kuwa masuala yote kuhusu huduma za miamala ya kifedha, na husimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Unashauriwa uwasiliane na BOT kwa kupitia namba 022 223 4494-97 ulizia Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa (NPS) kwa ajili ya muongozo sahihi na kwa haraka. Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au kwa kuandika baruapepe dawatilahuduma@tcra.go.tz.
Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.
Wasilisha lalamiko lako kwa Mtoa Huduma wako kwa njia ya maandishi aidha kwa barua au baruapepe na pale usipo pata jibu ndani ya siku 30 au ukipata jibu usiloridhika nalo. Unapaswa kuwasilisha lalamiko lako TCRA na viambatanisho vya ushahidi wa kuwasilisha lalamiko lako kwa Mtoa Huduma wako. Kwa maelezo zaidi tupigie simu kupitia namba 0800008272 (bila malipo).
Kwa maelezo zaidi tupigie simu kwa namba 0800008272 (bila malipo) au tuandikie barua pepe kwa anwani ya dawatilahuduma@tcra.go.tz. Asante kwa kuwasiliana na TCRA.
Kufanya utapeli mtandaoni ni kutenda kosa la jinai. Kosa la jinai ni tendo lolote ambalo limekatazwa kwa Sheria ambapo mtu yeyote akilitenda anakuwa ameikosea Jamhuri. TCRA hushirikiana na Jeshi la polisi kuhakikisha watu wanaojihusisha na utapeli mtandaoni wanabainishwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.



