Piga simu dawati la huduma, namba 0800008272 au tuma barua pepe kwenda: nms@tcra.go.tz.
Huduma ya mtumiaji kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba yake ya simu, yaani kwa kifupi MNP inakuwezesha kubakia na namba yako ya simu ya mkononi iwapo utaamua kubadili mtoa huduma za simu za mkononi Tanzania. Kimsingi; inakuwezesha kuendelea kutumia namba yako ya simu ya mkononi hata unapohamia mtandao mwingine. Kwa hiyo iwapo utabadili mtoa huduma za simu za mkononi, namba yako itabakia ile ile na hutahitajika kusumbuka kuwataarifu marafiki/familia/jamaa zako kuhusu mabadiliko ya mtoa huduma.
Ndani ya siku 14 za kazi.
Ufuatao ni utaratibu wa kuomba raslimali za namba kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Namba, yaani NMS:
i. Fungua akaunti kwa kujisajili kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Namba.
2. Jaza wasifu wa Kampuni/Taasisi na ambatanisha nyaraka husika kama vile nakala iliyoidhinishwa ya Cheti cha usajili wa kampuni, Namba ya Mlipa Kodi na Katiba ya Kampuni.
3.Endelea na kujaza fomu ya maombi kwa kuchagua kipengele kinachohusika (mfano, Mpya, Kuongeza muda au Kubatilisha Maombi).
4. Kamilisha fomu ya maombi mtandaoni na wasilisha, kisha fuata maelekezo kutoka NMS kupitia taarifa zitakazotumwa kwako kuitia barua pepe uliyoiweka.
Hapana; ni lazima muombaje awe kampuni, Asasi isiyo ya Kiserikali, Taasisi ya Serikali au mwenye leseni ya Huduma za Programu Tumizi kutoka TCRA.
Yeyote mwenye leseni ya Mawasiiano ya Kielektroniki (mfano wenye mitandao ya mawasiliano ya simu za mkononi) au hata wengine kama vile Kampuni, Taasisi ya Serikali na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs).
Mfumo wa Usimamizi wa Namba unafikiwa kupitia tovti ya TCRA ambayo ni: https://www.tcra.go.tz/ au moja kwa moja kwenye: https://nms.tcra.go.tz:32443/nms/
Maombi yote ya raslimali za namba za mawasiliano yanafanyika mtandaoni kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Namba, yaani Numbering Management System au kwa kifupi NMS, ambao unapatikana kwenye tovuti ya TCRA, ambayo ni: https://www.tcra.go.tz/
- Kutoa majina na anwani, yaani kufikisha simu na ujumbe kwa mtumiaji husika au mahali husika ndani ya mtandao;
- Kuwapatia wanaopiga simu mwekeleo wa gharama zitakazotumika katika kupiga simu kwenye namba husika; mfano taarifa zinazoelezea kikamilifu eneo la kijiografia na gharama za kupiga simu kwenye mtandao wa mtumiaji na nje ya mtandao wake.
- Zinawawezesha watoa huduma kupanga viwango vya kutoza kwa mtumiaji mmojammoja au vya jumla (yaani gharama za maunganisho ya simu kati ya mitandao).
- Kuweza kufuatilia simu zinazopigwa, kutambua simu zenye malengo maovu, kuzuia na kutambua ulaghai.
- Kuweka na kutambulisha aina za huduma (mfano huduma na taarifa vinavyotolewa bila malipo) na watoa huduma na mitandao mahsusi.
Namba ni raslimali muhimu katika utoaji wa huduma kwa watumiaji na katika kuendeleza ushindani na ubunifu katika huduma za mawasiliano ya simu. Watoa huduma za mitandao wanahitaji namba ili kutoa huduma za mawasiliano ya sim kwa watumiaji. Huduma hizo ni pamoja na:
- Simu za mezani;
- Simu za mkononi;
- Hduma za mawasiliano ya simu kupitia intaneti;
- Misimbo mifupi, ikiwa ni pamoja na ile inayotumika kwenye huduma za dharura (mfano 112 ya polisi) na huduma kwa wateja (mfano 100);
- Huduma za ziada za taarifa, huduma za kifedha na huduma za serikali;
- Premium Rates Services (PRS);
- Namba za bure (zisizolipiwa); na
- Mawasiliano kati ya mashine na vifaa vilivyounganishwa kwenye intaneti



