TCRA

TCRA

Creating a Level Playing Field

Initializing...

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Pata majibu kwa maswali ya kawaida yanayohusu mada mbalimbali.

EMF "ElectroMagnetic Fields" ni dhana inayohusiana na sumaku-umeme. Vifaa vyote vya umeme au elektroniki vinazalisha sumaku-umeme. Vyanzo vya kawaida vya EMF ni pamoja na kompyuta, televisheni, ovena za maikrowevu, vifaa visivyotumia waya kama simu za mkononi na vifaa vya Wi-Fi, laini za umeme, mifumo ya waya katika majumba, paneli za umeme, transfoma, mota na aina zote za mifumo ya utangazaji, ikiwa ni pamoja na redio za AM na FM.

Pia, masafa na mifumo ya mwanga ya kawaida ni aina za EMF. Mbali na mwanga wa kawaida unaoonekana, aina nyingine za mwanga zisizoonekana kama vile mialekundu (infrared), na Urujuanimno (ultraviolet), eksrei na mionzi ya gamma ni aina za EMF.