TCRA inamtambua mmilki wa domeini kama kampuni au mtu binafsi iliyoweka/aliyewekwa kwenye kanzidata ya rajisi kama msajiliwa wa domeini wakati wa usajili wa domeini.
Iwapo kampuni au mtu binafsi inatumia/anatumia mtu mwingine au wakala kusajili majina ya domeini yake, sharti wahakikishe kwamba wameonyeshwa kama wanaosajiliwa kwa domeini husika na si vinginevyo.
Kwa kawaida ada za mwaka za domeini zinalipwa kila mwaka tarehe ambayo domeini ilisajilliwa. Iwapo ana za mwaka hazitalipwa, domeini itaingia ngazi ya kumalizika muda wake, ambapo taarifa itatumwa kwa mhusika wa kuendesha domeini na mwenye domeini aliyesajiliwa. Siku 30 baada ya ngazi ya domeini kumalizika muda, domeini itapelekwa kwenye ngazi ya Kutolewa, yaani Out-of-zone (OOZ), ambamo domeini itabakia kwenye kanzidata ya rajisi lakini haitapatikana kwenye mfumo wa DNS. Wakati domeini ikiingia kwenye ngazi ya OOZ, taarifa itatumwa wakati huo huo kwa mhusika wa kuendesha domeini na mhusika wa masuala ya kiufundi. Domeini itabakia kwenye ngazi ya OOZ kwa siku 30 zaidi kabla haijafutwa. Baada ya kufutwa, domeini itaondolewa moja kwa moja kutoka kwenye kanzidata ya rajisi na hapo hapo inapatikana kwa ajili ya usajili na mhusika mwingine anayesajiliwa.
Mhusika wa masuala ya kiufundi anawajibika kwenye kuendesha na kusasisha kompyuta zinazohifadhi taarifa za Mfumo wa vikoa ambazo zinahusika na jina la domeini
Mhusika wa kuendesha domeini anaidhinishwa na yule anayesajiliwa kuwasiliana na rajisi (TCRA) au msajili wa majina ya domeini kujibu maswali kuhusu usajili wa majina ya domeini na anayesajiliwa.
Ndio; iwapo anayesajiliwa haridhiki na huduma za msajili aliye naye, yuko huru kuhamisha domeini zake kwa msajili mwingine wanayemtaka.
Utaratibu uliowekwa wa kuwasilliana na domeini unahitajika katika kuulizia na kufuatilia msimbo wa kuhamisha domeini kutoka kwenye rajisi, ama kwa kupitia sehemu ya tovuti ambamo mhusika anajihudumia mwenyewe kwenye tovuti ya https://karibu.tz au kwa maandishi kwenda kwenye rajisi kupitia rajisi@tcra.go.tz.
Ufunguo wa Rajisi ya Jina la Domeini unajulikana pia kama Nywila ya Domeini. Ni nywila yenye msimbo uliochanganywa ambayo inakutruhusu kuhamisha Jina la Domeini kwenda kwa Msajili mwingine.
Ndiyo; kuanzia tarehe 1 Machi 2022, wanaosajiliwa wataruhusiwa kusajili domeini moja kwa moja chini ya domeini ya kiwango cha juu ya fumbo ya dot tz; kama vile karibu.tz. Domeini hizi zinajulikana kama domeini za kiwango cha juu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejea Mwongozo wa Usajili wa domeini za ngazi ya Pili ambao unapatikana: https://karibu.tz/.
Ada za majina ya domeini zinapatikana kwenye kiambatanisho cha pili cha Kanuni za Mawasiliano ya Kielektoniki na Posta (Usimamizi wa Majina ya Domeini) za 2020. Ili kuunganishwa na kuona bofya: https://karibu.tz/media/regulations.pdf
Orodha ya wasajili walioidhinishwa inapatikana kwenye kwenye tovuti ya Karibu. Ili kuunganishwa na kuona orodha, bofya kwenye: https://karibu.tz/domains/registrars/
Unaweza kusajili majina ya domeini kwa kuchagua mmojawapo wa wasajili walioidhinishwa na ambao wamechaoishwa kwenye sehemu iliyoko kwenye tovuti ya Karibu. Ili kuunganishwa na kuona orodha, bofya kwenye:. https://karibu.tz/domains/packages/
Majina ya Domeini ya ya Fumbo ngazi ya Pili ni kama ifuatavyo:
- <jina>.co.tz – kwa taasisi yoyote, ikiwa ni pamoja na kampuni au biashara zilizosajiliwa;
- <jina>.or.tz – taasisi zisizojiendesha kibiashara;
- <jina>.go.tz – domeini iliyotengwa kwa taasisi za Serikali ya Tanzania kama zinavyotambuliwa kupitia Bunge au kwa kuwa na barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara husika ilipo taasisi hiyo;
- <jina>.ac.tz– domeini iliyotengwa kwa vyuo vya elimu au taasisi za ufundi zenye usajili kama ipasavyo;
- <jina>.ne.tz – kwa mtandao wa watu au bidhaa;
- <jina>. mil.tz – domeini iliyotengwa kwa taasisi za kijeshi za Tanzania zinazotambuliwa na Wizara yenye majukumu ya Ulinzi.
- <jina>.sc.tz – domeini iliyotengwa kwa shule za awali, msingi na taasisi za ngazi ya sekondari;
- <jina>. info.tz – kwa domeini zinazotoa habari kuhusu masuala mahsusi;;
- <jina>.tv.tz – kwa matumizi ya watunza maudhui, watengenezaji wa filamu na stesheni za televisheni;
- <jina>. mobi.tz – kwa watoa huduma kupitia vifaa vya mkononi;
- <jina>. hotel.tz – kwa watoa huduma za malazi na ukarimu; na
- <jina>.me.tz – kwa watu binafsi.
Meneja (ccTLD) ni taasisi (kampuni) au mtu binafsi ambaye anashughulikia masuala ya kila siku ya Domeini ya Kiwango cha juu ya Fumbo au shughuli zinazoambatana nayo kwa niaba ya jumuiya ya intaneti alipo.
Mamlaka inayokasimu majukumu kwa Meneja wa Domeini ya Kiwango cha juu ya Fumbo ni taasisi ya kimataifa inayosimamia masuala ya intaneti, inayoitwa ICANN, ambacho ni kifupisho cha Internet Corporation for Assigned Names and Numbers.
Kwa kikoa cha dot tz (.tz) cha ccTLD, meneja ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Huyu ni taasisi au mtumiaji binafsi ambaye anasajili kikoa.
Ni mtu au taasisi iliyopewa kibali na Mamlaka kusajili, kufuta, kuongeza, kurekebisha au kubadili vikoa chini ya utaratibu wa vikoa vya dot tz (.tz).
Rajisi inafanya kazi kama hazina ya yenye mamlaka inayohifadhi taarifa zote zinazotakiwa kutoa ufumbuzi wa vikoa vilivyosajiliwa kwenye domeini ya kiwango cha juu ya fumbo (TLD) na rajisi hiyo au domeini za ngazi ya pili (SLDs) iwapo mfumo wa SLD unatumika (kwa mfano co.tz, ac.tz).
Rajisi hiyo pia inaweka taarifa za ziada kama vile uendeshaji wake na utaratibu wa kiufundi wa kuwasiliana nayo, namna ya kuwasiliana na domeini husika, utaratibu wa mawasiliano kwa ajili ya ankara na mrajisi aliyesajili kikoa hicho.
Domeini ya Kiwango cha Juu ya Fumbo la Nchi, (kwa ufupi ccTLD) ni domeini ya kiwango cha juu ya fumbo ambacho kawaida kinatumika au kimetengwa kwa nchi, dola huru au eneo la nchi linalotambulika kwa msimbo wa nchi.
Domeini ya kiwango cha juu ya fumbo ina urefu wa herufi mbili; kwa mfano TZ ni Tanzania, KE ni Kenya, UK ni Uingereza.
Kwa lugha nyepesi, mfumo wa vikoa, au DNS in kitabu cha namba za mawasiliano kwa intaneti, unaounganisha watumiaji wa mtandao wa intaneti na tovuti mballimbali.
Mfumo wa vikoa, yaani DNS ni kanzidata iliyojengeka na duniani na ambayo inawezesha mawasiliano kupitia intaneti kwa kutafsiri majina haya ambayo ni rahisi kutumia (vikoa) kuwa misimbo mifupi ya namba (anwani za intaneti) ambazo kompyuta au vifaa vinavyotumika kwenye mtandao vitazielewa; na kinyume chake.
Ni jina mahsusi linalotambua raslimali za intaneti kama vile tovuti zilizosajiliwa nchini na ngazi nyingine duniani.
Kompyuta zilizounganishwa kwenye intaneti zina anwani za namba mahsusi zinazoziwezesha kufikisha taarifa za kielektroniki mahali sahihi. Mfumo wa Majina ya domeini (DNS) unatafsiri anwani hizo za namba kwenye kompyuta na kuzipa majina ambayo ni rahisi kutumiwa. Vikoa vinavyojitokeza ni rahisi kukumbuka na vinasaidia watu kupata taarifa kwenye intaneti.
Vikoa vinatumika kutambua kurasa mahsusi za tovuti. Kwa mfano, katika anwani ya tovuti ya "https://www.tcra.go.tz," kikoa ni tcra.go.tz.
Vikoa pia vinatumiwa katika anwani za barua pepe ambazo zinawezesha watu kutuma na kupokea ujumbe wa kielektroniki; kwa mfano, barua@tcra.go.tz.



