TCRA inahusika moja kwa moja katika kudhibiti Watoa Huduma za Mawasiliano nchini.
Zipo sababu nyingi ambazo husababisha vifurushi vya Mawasiliano kuisha ghafla au haraka kabla ya muda uliobainishwa. Miongoni mwa sababu ni uwezo wa simu janja unayotumia, mathalani kama ni simu ya kisasa, yenye uwezo mkubwa na kasi ya juu. Pia, kutozifunga aplikesheni ambazo umezitumia, kuacha wazi kitufe cha ‘location’, na kuacha wazi kitufe cha roaming. Sababu nyingine ni kuongezeka kwa kasi ya internet, na kuwa na aplikesheni nyingi kwenye simu. Kiwango cha matumizi ya data kinategemea sana udhibiti wa mtumiaji wa kifaa cha Mawasiliano kiganjani; iwapo utahisi./p>
Kuhujumu miundombinu ya mawasiliano ni kutenda kosa la jinai. Kosa la jinai ni tendo lolote ambalo limekatazwa kwa Sheria ambapo mtu yeyote akilitenda anakuwa ameikosea Jamhuri. TCRA hushirikiana na vyombo vya dola vyenye jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria, likiwemo Jeshi la Polisi ilikuchunguza,kukamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wanaobainika kuhujumu miundombinu ya mawasiliano. Hivyo, ni wajibu wa kila mwananchi, kulinda miundombinu ya mawasiliano na kujiepusha na matendo ya jinai dhidi ya miundombinu ya mawasiliano.



